Saturday 3 February 2018

AMIRI JESHI MKUU RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA192 WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA PAMOJA NA BAADHI WA NCHI MARAFIKI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kutunukiwa Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli (TMA) Meja Jenerali Paul Peter Masao katika picha ya pamoja na Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki mara baada ya kuwatunuku Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati Bendi ya Jeshi la Ulinzi ilipokuwa ikitoa burudani katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuisha kwa shughuli za Kutunuku Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kutunuku Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki. PICHA NA IKULU

SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.
Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Alisema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.
“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima.”

Alitoa mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”

Alisema kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea sana msaada wa Serikali. “Soko la Bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”

Bw. Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wanamatumaini makubwa kwamba soko hilo litatimiza malengo yake.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, FEBRUARI 3, 2018.

SHERIA MPYA YA MADINI YA MWAKA 2017 INATAKA KURUDISHA UCHUMI KWA WANANCHI: MHE BITEKO

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo amesisitiza viongozi kusimamia Kanuni na taratibu juu ya usimamizi wa madini, leo 3 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Kahama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Fadhil Nkulu wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alipozuru Wilayani humo kwa ziara ya kikazi, Leo Februari 2018.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga aakiwa katika ziara ya kikazi, leo 3 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Shinyanga
"Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inataka kurudisha uchumi wa madini kuwa uchumi fungamanishi kwa sekta nyingine, Hatuwezi kuwa na Mgodi ndani ya nchi ambao ajira zote zinapelekwa nje ya nchi kupitia huduma mbalimbali, unaweza kuagiza bidhaa za kila aina kutoka nje ya nchi lakini huwezi kuagiza ajira za wananchi wako zitoke nje kuja ndani, kamwe haiwezekani"

Ni Kauli ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 3 Februari 2018 wakati akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo amesisitiza zaidi viongozi wa serikali katika maeneo yao kusimamia Kanuni na taratibu juu ya usimamizi wa madini.

Mhe Biteko alikaririwa akisema kuwa usimamizi madhubuti wa sheria na taratibu zilizowekwa ni sehemu imara na makini itakayowanufaisha watanzania ambapo watakuwa wamemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ambaye amejidhatiti kwa mtazamo wa kuwanufaisha watanzania kupitia rasilimali zao.

Kanuni ya madini ya mwaka 2018 imeelekeza kuwa mgodi wowote unapoanza asilimia 100% za watoa huduma za chakula wanapaswa kuwa watu wa wananchi wa Tanzania, Pia huduma za ulinzi kwa asilimia 100% zinapaswa kutolewa na kampuni za ndani. Hivyo wataalamu wa sekta ya madini ni lazima kusimamia Kanuni hizo kwa usahihi.

Mhe Biteko aliongeza kuwa kampuni ya kigeni inaweza kufanya huduma hizo lakini ni lazima iingie ubia na wananchi wa Tanzania na kanuni hizi serikali imeziweka kwa makusudi kabisa ikiwa na mtazamo wa kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao.

Mhe Biteko alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho kimeingia mkataba na wananchi katika kuwatumikia kwa usimamizi madhubuti kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 hivyo viongozi wa CCM wanapaswa kusimamia vyema serikali ili kuongeza tija katika utendaji.

Sambamba na CCM kusimamia vyema serikali pia Naibu Waziri huyo wa Madini amewataka watendaji wote wa serikali kuwa na umoja katika utendaji wao kwa usimamizi madhubuti wa rasilimali madini huku akitoa onyo Kali kwa watendaji wa serikali, Viongozi, vyama vya siasa na wananchi kujihusisha na rushwa kwani kufanya hivyo ni kuzififisha juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli ya kuwainua wananchi wanyonge ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali zilizopo.

"Ndugu zangu ni aibu mno dhahabu na madini yetu mengine kuchimbwa nchini lakini yanajenga nchi nyingine, Uhakika wa barabara bado hatuna katika maeneo mengi, maji bado hatuna, sekta ya afya haijaimarika, Zahanati zina shida lakini pia Karibu kila maeneo hatujajidhatiti kwa asilimia 100% Kwa hiyo Mhe Dc naomba sana msicheke na mtu yeyote anayecheza na rasilimali zetu This Must be a Serious business, Mimi najua we have the same spirit lazima tufanye kazi kwa weledi.

LSF YAKUTANA NA WADAU WA WATOA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA, JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Muda wa Asasi ya kiraia ya Legal Services Facilities (LSF) Dkt. Benson Bani , akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya LSF Bw. Kees Groenendijk akitoa mada yake ambapo alizungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelezea malengo, mambo mbalimbali yaliyofanyika kwa mwaka 2017 pamoja na mwelekeo kwa mwaka 2018, wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.Meneja Miradi wa LSF Bw.Ramadhani masele akielezea kiundani juu ya utendaji , mrejesho na nini kifanyike wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.

Baadhi ya wakurugenzi na wajumbe wa Bodi za ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakitoa maoni mbalimbali wakati wa warsha hiyoAfisa ufuatiliaji na tathimini kutoka LSF Bi. Saada Mkangwa akitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa taarifa za wanufaika wa ruzuku.Mkurugenzi wa miradi wa LSF Bi. Scholastica Julla akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.