Siku hii haikupaswa kufika huku; lakini imefika na historia inabakia historia. Zitto Kabwe aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara) amejivua uanachama (au amekubali kuvuliwa uanachama kulikotangazwa na CC ya chama) na hivyo kupoteza pia Ubunge wake. Wananchi wa Kigoma Kaskazini sasa hawana muwakilishi na hawatokuwa na mwakilishi kipindi kizima cha Bunge lililobakia (hasa Bunge la mwisho la Bajeti kabla ya Uchaguzi Mkuu).
Kauli yake mwenyewe katika kile ambacho kilitarajiwa kufanyika jana katika "Hotuba Niliyotaka Kutoa":
Na Barua yake ya kuondoka Bungeni:Mheshimiwa Spika, Kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika dhamira kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, yaani Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.
Ni wazi pia inaonekana tayari anaangalia chama kingine kujiunga nacho siku chache zijazo. Swali kubwa linabakia ni je hili litakuwa na matokeo ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiyakisia kuhusiana na kugawanya chama au nalo litapita?
Vyovyote vile ilivyo ni lazima tukubali kuwa yote yaliyotokea ni sehemu ya siasa zetu. Swali moja ambalo ameliibua na ambalo sisi kama taifa tunahitaji kulifanyia uamuzi mapema ni hili la kulazimisha wabunge kuwa wanachama wa vyama vya siasa na kuwa chama cha siasa kinaweza kumfutia mtu uanachama na akapoteza Ubunge wake. Ni lazima tutafute balance kati ya nidhamu ya chama (party discipline) na utumishi wa kisiasa. NI vizuri labda tuangalie namna ya kuweza kumfukuza mbunge Bungeni (hili lipo) bila kumfutia uanachama. Lakini kwenye Bunge ambalo lina wabunge wengi wa chama kimoja itakuwa Mbunge waupinzani akakubaliwa na Bunge la chama hicho lakini akashindwa kuondolewa na chama chake?
Ni muhimu kuwa na ubunifu wa aina fulani. Lakini pia sakata zima la Zitto linaacha tamanio moja la kutaka viongozi au wale wanaoitwa kuwa ni viongozi kujaribu kuonesha umakini wa kutatua migogoro mapema zaidi kabla haijafikia mafuriko.
Friday, 20 March 2015
Thursday, 19 March 2015
TANZANIA YAPITISHA MUSWADA WA AJIRA
Bunge
la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za
wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha
vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo
limesisitiza serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini
uwezo kuhusu ajira wazoomba na mienendo yao kijamii.
Sheria hiyo pia inawataka watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana
na sifa zao.huku wageni wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji
ili kuleta ushindani sahihi katika soko la ajira nchini humo.
Sheria hiyo inalenga kuvutia waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana
na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa wazawa.Akichangia muswada huo
kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse anaeleza jinsi wazawa
wanavyopaswa kunufaika zaidi
Gaudensia Kabaka ni waziri wa kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema
kuwa vibali vya kazi kwa wageni na suala la uraia kwa mjibu wa sheria
hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali kinachotakiwa ni kutumiza
masharti yote mawili.
Kupitia muswada huu,bunge limesema kuwa ni moja ya hatua itakayosaidia
ajira wa vijana wa Tanzania ambayo baadhi yao wanakosa ajira kutokana na
mazingira ya kipaumbele kuwa kwa wageni na si wazawa kama ilivyo katika
mataifa mengi duniani ambayo kutoa fursa kwa wenyeji na kisha wageni
baadaye.
Wednesday, 18 March 2015
WAZEE MANISPAA YA BUKOBA WAMUOMBA BALOZI KAGASHEKI ACHUKUE FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE.
Wazee katika Manispaa ya Bukoba kwa kauli moja wamemuomba Mh Balozi Khamis Sued Kagasheki kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Bukoba,Katika hotuba ya ufunguzi Katibu wa wazee MZEE Haruna Almasi alieleza kwa kina namna walivyoridhishwa na utendaji wa kazi wa mbunge katika kipindi chake cha uongozi na kutamka kuwa amejitaidi sana katika swala la kuleta maendeleo na kuhakikisha anatetea haki za wanyonge bila woga, na hata pale wabaya wake walipojaribu kubadilisha ukweli na kumzushia bado alisimama na kudai haki za wanyonge bila woga kwa kujari haki za wanachi. Kwa mantiki hiyo wote kwa kauli moja wamemuomba agombee tena kwa kipindi kingine, na wao kama wazee kwa nafasi yao watahakikisha chama cha mapinduzi kinashinda,Pia Bw Haruna amewataka wanaccm wote kwa ujumla wao kuhakikisha wanaondoa tofauti zao na kuakikisha kila mmoja kutambua wajibu wake wa kutetea chama cha mapinduzi.
Wazee kutoka maeneo mbalimbali wakiwa ukumbini.
Mh Balozi Khamis Kagasheki akiongea na wazee.
Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera.
Mzee Byolwango akiwa na Haji Abas
Dk Kalumuna akichangia mada.
Mzee Kikwemu .
Kamanda wa uvccm Bukoba Mjini Philbert Nyerere akiongea na wazee.
Katibu wa ccm Mkoa akiongea na wazee.
Katibu wa ccm wilaya akisisitiza wazee wajiandikishe katika daftari la kudumu la kupiga kula.
Wazee kutoka maeneo mbalimbali wakiwa ukumbini.
Mh Balozi Khamis Kagasheki akiongea na wazee.
Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera.
Mzee Byolwango akiwa na Haji Abas
Dk Kalumuna akichangia mada.
Mzee Kikwemu .
Kamanda wa uvccm Bukoba Mjini Philbert Nyerere akiongea na wazee.
Katibu wa ccm Mkoa akiongea na wazee.
Katibu wa ccm wilaya akisisitiza wazee wajiandikishe katika daftari la kudumu la kupiga kula.
Tuesday, 17 March 2015
KAGASHEKI KUUNGURUMA UWANJA WA UHURU PLATFORM BUKOBA MJINI JUMAMOSI 21-3-2015 KUANZI SAA TISA ALASIRI
Monday, 16 March 2015
FALCON WALETA MABASI MAPYA KWA SAFARI ZA BUKOBA - DAR KILA SIKU.
Usafiri ni moja ya huduma muhimu sana katika jamii,Kampuni ya mabasi ya Falcon wametambua hilo na kuhakikisha katika jitihada za kutoa huduma bora wameleta mabasi mapya kwa ajiri ya kusafirisha abiria kila siku Bukoba - Dar kila siku kwa gharama nafuu.
Muonekano wa mabasi.
Sehemu ya ndani ya Basi.
Viti vya kujinafasi.
Dereva.
Abiria kwa raha zao.
Ukiwa safarini utapatiwa kinywaji cha kukuburudisha, huku ukitazama Tv.
Ni ofisi za Falcon zipo stand kuu ya Mabasi Bukoba, safari kwa raha na Falcon.
Muonekano wa mabasi.
Sehemu ya ndani ya Basi.
Viti vya kujinafasi.
Dereva.
Abiria kwa raha zao.
Ukiwa safarini utapatiwa kinywaji cha kukuburudisha, huku ukitazama Tv.
KINANA AITEKA KARATU
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Karatu mjini katika viwanja vya Mazingira Bora.
Kinana
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara ikiwa moja ya sehemu ya
mpango wa ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama, kukagua na
kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
Kinana akihutubia wananchi wa Karatu ambao wamechoka utawala wa wapinzani Karatu mjini
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Karatu na kuwaambia Upinzani umekwisha Karatu.
Vijana wa mjini wanakuambia ukiona nyomi kama hili lime jaa katika mkutano wa CCM kartau mjini ujue upinzani kwa heri.
..
Subscribe to:
Posts (Atom)