Wednesday 18 March 2015

WAZEE MANISPAA YA BUKOBA WAMUOMBA BALOZI KAGASHEKI ACHUKUE FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE.

 Wazee katika Manispaa ya Bukoba kwa kauli moja wamemuomba Mh Balozi Khamis Sued Kagasheki kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Bukoba,Katika hotuba ya ufunguzi Katibu wa wazee MZEE Haruna Almasi alieleza kwa kina namna walivyoridhishwa na utendaji wa kazi wa mbunge katika kipindi chake cha uongozi na kutamka kuwa amejitaidi sana katika swala la  kuleta maendeleo na kuhakikisha anatetea haki za wanyonge bila woga, na hata pale wabaya wake walipojaribu kubadilisha ukweli  na kumzushia bado alisimama  na kudai haki za wanyonge bila woga kwa kujari haki za wanachi. Kwa mantiki hiyo wote kwa kauli moja wamemuomba agombee tena kwa kipindi  kingine, na wao kama wazee kwa nafasi yao watahakikisha chama cha mapinduzi kinashinda,Pia Bw Haruna amewataka wanaccm wote kwa ujumla wao kuhakikisha wanaondoa tofauti zao na kuakikisha kila mmoja kutambua wajibu wake wa kutetea chama cha mapinduzi.
 Wazee kutoka maeneo mbalimbali wakiwa ukumbini.
 Mh Balozi Khamis Kagasheki akiongea na wazee.
 Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera.
 Mzee Byolwango akiwa na Haji Abas
 Dk Kalumuna akichangia mada.
 Mzee Kikwemu .
 Kamanda wa uvccm Bukoba Mjini Philbert Nyerere akiongea na wazee.
 Katibu wa ccm Mkoa akiongea na wazee.
Katibu wa ccm wilaya akisisitiza wazee wajiandikishe katika daftari la kudumu la kupiga kula.

No comments:

Post a Comment