Bunge
la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za
wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha
vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo
limesisitiza serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini
uwezo kuhusu ajira wazoomba na mienendo yao kijamii.
Sheria hiyo pia inawataka watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana
na sifa zao.huku wageni wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji
ili kuleta ushindani sahihi katika soko la ajira nchini humo.
Sheria hiyo inalenga kuvutia waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana
na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa wazawa.Akichangia muswada huo
kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse anaeleza jinsi wazawa
wanavyopaswa kunufaika zaidi
Gaudensia Kabaka ni waziri wa kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema
kuwa vibali vya kazi kwa wageni na suala la uraia kwa mjibu wa sheria
hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali kinachotakiwa ni kutumiza
masharti yote mawili.
Kupitia muswada huu,bunge limesema kuwa ni moja ya hatua itakayosaidia
ajira wa vijana wa Tanzania ambayo baadhi yao wanakosa ajira kutokana na
mazingira ya kipaumbele kuwa kwa wageni na si wazawa kama ilivyo katika
mataifa mengi duniani ambayo kutoa fursa kwa wenyeji na kisha wageni
baadaye.
No comments:
Post a Comment