Kikosi
cha wawakilishi watanzania katika michuano ya kimataifa ya kombe la
Shirikisho barani Afrika Yanga wamewasili salama nchini Algerai kwa
ajili ya mchezo wao marudiano dhidi ya MC Alger utakaochezwa kesho
majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika
msafara huo uliiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa
umefika salama na ukipokelewa na watanzania wanaoishi nchi Algeria na
kufurahishwa na mapokezi hayo na kuahidi ushindi kwa watanzania.
Msafara
wa wachezaji hao uliingia kwa mafungu mawili ambapo kundi la kwanza
liliwasili likiongozwa na benchi la ufundi la timu hiyo likiwa na kocha
Mkuu George Lwandamina huku kundi la pili likiwasili na Katibu Mkuu.
Mtanzania
Hamis Mwampese anayeishi nchini Algeria amesema kuwa timu ya Algers
wameingia uoga hasa baada ya kuona Yanga wamechelewa kuingia nchini humo
na zaidi kwa kufanya hivyo wameepusha sana kufanyiwa hujuma na wenyeji
wa nchi hiyo.
Yanga
wamefikia katika Hotel ya nyota tano inayojulikana kwa jina la Sultan
ambapo si mbali sana na Uwanja ulipo utakaochezewa kesho katika mechi
hiyo ya marudiano ambapo Yanga wanatakiwa kupata ushindi wa aina yoyote
au sare.
Mtanzania Hamis Mwampese akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa baada ya kuwasili Jijini Algeria kwa
ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho
barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga
walitoka na ushindi wa goli 1-0..
Mtanzania
Hamis Mwampese akiwa katika picha mbalimbali na wachezaji wa timu hiyo
baada ya kuwasili nchini Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano ya
hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger
ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0.