Saturday 29 June 2013

MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 APATIKANA NI LUCY CHARLES KUTOKA MWANZA. OMMY DIMPOZ NA MICHAEL ROSS WAKIWASHA MOTO!

Mrembo Lucy Charles akitabasamu baada ya kuvikwa taji la Redd's miss Kanda ya Ziwa usiku huu.

Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 17 waliojitokeza.

Mrembo huyo aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Hotel ya Gold Crest baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Eshe Rashid  na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore

Vinara watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's miss Lake zone 2013, kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha Isdore kutoka Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga


Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba(kushoto) na kulia ni Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wakiwa ni wageni rasmi
KIushoto ni Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akiwa na wageni wengine kulia.
Show ya ufunguzi kwa warembo ikaanza
Warembo wakionesha vipaji vyao

Furaha ikitanda kwa kila mmoja
eee..na yule yumo...!!!
Kila mrembo akiesha uchezi wake hapa na makeke zaidi ..kiufundi kujitengenezea nafasi ya kushinda taji
Baadhi ya mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Hotel ya Gold Crest
Hapa kila mmoja alikuwa na wake wa kumchangua na kila mmoja akijiuliza swali nani kutwaa taji !!
Jamal Kalumuna kutoka Bukoba akiwa na furaha baada ya kuwaona warembo jukwaanin
Meza kuu Viongozi mbalimbali

Mwandaaji wa Miss Redd's Lake Zone 2013 akisikiliza neno kutoka kwa  Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
Mc Kulia akiwa na Mwandaaji ambaye anahusika na Swala zima na akiwa anatoka Clara Salon & Boutique Bi Clara Mwassa.
Furaha zikapenya kwa Viongozi hawa ambao ndiyo walikuwa majaji
Usipime!!!...
Mashidonge- akicheza na Moto kwenye ukumbi huu wa Gold Grest Hotel
Umati wa watu ukimwangalia kwa makini Mashidonge wakati anacheza na Moto usiku huu.
Mashidonge akitengeneza alama jukwaani!!...
Full Mzuka!!
Michuzi ikimfata alipo!!
Miss Talent naye akuwa Nyuma Babylove Kalalaa akaanza kuonesha vitu vyake ...kipanji toka moyoni.Babylove Kalalaa akiwa na nyoka wake jukwaani kuwapagawisha mashabiki wake.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba ilibidi asimame maana ilikuwa kazi kweli kweli na kwa mara ya kwanza namuona na yeye anachukua kumbukumbu kwenye simu yake.!!
matukio ..tunachukua na sisi...
Babylove Kalalaa akijikusanyia makato!!
Mnataka tena jamani!!!
warembo wote wakaitwa !!






Kiongozi wa BHATT ELECTONICS LTD Akiteta baada ya kuchagua warembo na kuwapatia kazi kwenye ofisi zao. Kumbuka BHATT ni wakala wa Samsung.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akijiandaa kuanza kuita 10 Bora hapa
Washiriki wote wazuri lakini tunataka kumi kwanza kisha tano!!
Top Ten hii hapa
Tano Bora

Ommy Dimpoz akitumbuiza
Ommy Dimpoz akishambulia jukwaa
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake
Tuendelee ama tusiendelee!!
Dadaz wakidata na nyimbo za mkali Ommy Dimpoz
Pongezi!!!
umefanya kazi kijana!!
Michael Ross Kutoka Uganda nae akaingia kwa mitindo ya aina yake!!
Dadaz wakimsonga Michael Ross kutaka kumshusha chini kucheza nae!
Raha jipe mwenyewe!!
...Omama yoyo!!



wewe tu ...nipe tano kwanza!!

kamata kitita chako Mrembo!!!
Zawadi zako hizi!!

ushindi  mtamu jamaniiii!
Picha ya pamoja Waandaji na majaji wa Redd's miss Lake zone 2013
Wanyange !!