Thursday 10 July 2014

KITUKO CHA MWAKA,BINT KAKUTWA KAUCHAPA USINGIZI NDANI YA SANDUKU LA CHIPS JIJINI DAR


Kwa haraka unaweza usiamini macho yako na hata ukibidi unaweza kuomba maji unawe uso ili uweze kuyaamini macho yako kile kinachoonekana mbele yako kama hivi.

Lakini baada ya kuamini macho yako bado unaweza kubaki na maswali mengi yasiyo na majibu, kwamba ni miujiza, Kiini macho au ni nini, na kubwa zaidi ni jinsi gani binti huyu anayeonekana kuwa ni mrefu kwa umbo amewezaje kuingia ndani ya Sanduku hili la Chips na kuenea na kuweza kujikunja kama hivi na kisha kuuchapa usingizi mnono bila shaka???.

Kiukweli unaweza kuwa eneo la tukio kwa muda wote hadi unaondoka na ukawa bado hujapata jibu la kujiridhisha na hasa unapokuwa ukisikia la kila mtu akisema yake kuhusiana na tukio hilo na ndivyo ilivyotokea juzi usiku huko eneo la Yombo jijini Dar es Salaam, ambapo Binti huyu alikutwa akiwa ameuchapa usingizi mzito ndani ya Sanduku lenye Chips na Mishikaki kibao.

Haikuweza kufahamika kwa haraka undani wa tukio hili. WADAU HIZI CHIPS HIZIIIIIII, KUWENI MACHO MTAJA KULA MISHIKAKI KUMBE NI YA JIMTU KAMA HUYU. Picha kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa.

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Filipe Nyusi alipowasili leo jioni Julai 9, 2014, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana
 Nyusi akidhihirisha furaha kwa mapokezi aliyopata

 Mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji akiwa na Mwenyeji wake, Kinana wakati wa mapokezi yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
 Filipe Nyusi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. 

 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere (watatulkushoto) akiwa na ugeni wa mgombea huyo wa Urais nchini Msumbiji, Filipe Nyus (wapili kushoto), nyumbani Mwalimu, Msasani, Dar es Salaam. Kushoto ni Kinana 
 Mama Maria Nyerere akimsalimia Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Machel, Samora Samora ambaye alifuatana na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji.
 Mama Maria Nyerere akizungumza na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji Filipe Nyus (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
 Nyusi na Kinana wakimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere wakati wa mazungumzo hayo
Samora Samora akizungumza na Binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wakati wa ugeni huo nyumbani kwa  Mama Maria Nyerere, Msasani Dar es Salaam.

Tuesday 8 July 2014

KANALI FABIANI MASSAWE AFUNGA MAONYESHO YA SABASABA BUKOBA

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanal Fabian Massawe ameyafunga rasmi maonyesho ya sabasaba 2014 yaliyoyanyika katika viwanja vya jengo la ccm Kagera.Maonyesho hayo yalioandaliwa na kampuni ya Kaidep wameshirikisha makampuni,Taasisi nawafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi Uganda,Rwanda,Burundi,Zaire naSudan.














 Mkuu wa Mkoa Fabin Massawe akitembelea mabanda