Thursday 10 July 2014

KITUKO CHA MWAKA,BINT KAKUTWA KAUCHAPA USINGIZI NDANI YA SANDUKU LA CHIPS JIJINI DAR


Kwa haraka unaweza usiamini macho yako na hata ukibidi unaweza kuomba maji unawe uso ili uweze kuyaamini macho yako kile kinachoonekana mbele yako kama hivi.

Lakini baada ya kuamini macho yako bado unaweza kubaki na maswali mengi yasiyo na majibu, kwamba ni miujiza, Kiini macho au ni nini, na kubwa zaidi ni jinsi gani binti huyu anayeonekana kuwa ni mrefu kwa umbo amewezaje kuingia ndani ya Sanduku hili la Chips na kuenea na kuweza kujikunja kama hivi na kisha kuuchapa usingizi mnono bila shaka???.

Kiukweli unaweza kuwa eneo la tukio kwa muda wote hadi unaondoka na ukawa bado hujapata jibu la kujiridhisha na hasa unapokuwa ukisikia la kila mtu akisema yake kuhusiana na tukio hilo na ndivyo ilivyotokea juzi usiku huko eneo la Yombo jijini Dar es Salaam, ambapo Binti huyu alikutwa akiwa ameuchapa usingizi mzito ndani ya Sanduku lenye Chips na Mishikaki kibao.

Haikuweza kufahamika kwa haraka undani wa tukio hili. WADAU HIZI CHIPS HIZIIIIIII, KUWENI MACHO MTAJA KULA MISHIKAKI KUMBE NI YA JIMTU KAMA HUYU. Picha kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa.

No comments:

Post a Comment