Friday, 14 March 2014

SHIDA HAINA MWENYEWE, MALAYSIA YATUMIA WAGANGA WA JADI KUTAFUTA NDEGE ILIYOPOTEA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCyu4OncJGxkOo_n-ny9PzS-D6H9aUB9uGj2HU3zkm9Iem6vipwHqgkALBCsh7smKXlY-RKvj5YTLYB7obHe_B9V6DckF-5yKQNNllB2TzxG9-SKTkv49h9Yg2lkeB81ygIe2HbNKoDug/s1600/malysia.pngWakati ambapo China imepeleka angani satellite 10 kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines iliyopotea, serikali ya Malaysia imewaomba waganga wa kienyeji kusaidia zoezi hilo.
Mganga maarufu nchini humo Ibrahim Mat Zin anayejulikana kama ‘Raja Bomoh Sedunia Nujum VIP’ alifanya tambiko kwenye uwanja wa ndege Kuala
Lumpur Jumatatu hii kusaidia kuitafuta ndege hiyo ya MH370. Anadaiwa kuitwa na viongozi wa juu wa serikali.

“Nadhani ndege bado ipo angani ama ilianguka baharini,” alisema Ibrahim Mat Zin. 

Thursday, 13 March 2014

SAMIA SULUHU HASSAN ACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akitoa shukrani zake kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akimkumbatia Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta Leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge Hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashilila akieleza wajumbe juu ya utaratibu wa upigaji kura kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti leo Mjini Dodoma.
 Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akinadi Sera zake  kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakibadilishana Mawazo na Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta(Aliyekaa).Leo mjini Dodoma.
Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akimpongeza Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutangazwa kuwa Makamu mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. 

SITA AIBUKA KIDEDEA KWA KURA 487 KATIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KUDUMU BUNGE LA KATIBA


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Hashim Rungwe akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa akiweka karatasi ya Kura yake ya Kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wakipiga Kura Kwa ajili ya Nafasi Ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Iliyokuwa Ikiwaniwa na Bw. Edward Lowasa na Bw. Hashim Rungwe leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa Kujitengemea, Hashim Rungwe. 

Sitta ameibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika leo jioni mjini Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda, Mh Ameir Pandu Kificho, amekabidhi madaraka hayo kwa mwenyekiti mpya Samuel Sitta baada ya kumaliza rasmi muda wake wa kuliendesha bunge hilo leo. 

Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiye mshindi wa kuanza kupambana na misukosuko ya bunge hilo ambalo kwa sasa litaanza kuendeshwa kwa kanuni.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wasira akiwa na Mjumbe mwenzie wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka wakati zoezi la upigaji kura likiendelea Leo Mjini Dodoma.

Wednesday, 12 March 2014

SITTA ACHUKUA FOMU KUWANIA UENYEKITI BUNGE LA KATIBA



Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akipokea Fomu kutoka kwa Ofisa wa Bunge Bi. Lidya Mwaipyana Katikati ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala.
Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akionesha fomu ya uenyekiti aliyochukua leo Kushoto niMjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala na Kulia ni Mjumbe wa Bunge hilo Bw. Paul Makonda.
Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya Kuchukua fomu hizo na kuahidi kufanya kazi kwa Kasi naViwango.

Sunday, 9 March 2014

HAFLA FUPI YA KUWAAGA MR & MRS ALFRED MATOVERO YAFANA

                            Mr & Mrs Alfred Matovero wakiingia katika ukumbi wa Lina's
 Ilikuwa ni hafla ya kuwaaga Mr & Mrs Matovero ambao wameamia mkoa wa Geita Kikazi
 Mkutubi wa kwanza kulia akiwa na tabasamu lililojificha
 Bety Nangai akimuonyesha kitu Lily Tigo
 Mama Nancy A.K.A Mama Matovero akisalimiana na Deo Rugaibura,hakika ilikuwa furaha
 Wakiwa katika eneo Rasmi lilioandaliwa kwa ajili yao
 Ni wadada warembo ambao walifanikisha hafla kupendeza, na kusababisha hata wale wenye haraka waendelee kuwepo
 Mtu mzima Super Mkude na Leoleo wakisakata rumba
 Mama Nancy akifungua shampein
 Watu walipendeza na kila mtu alionyesha upendo
 Wote macho kwangu, ni super mkude akisakata rumba
 Mkutubi
 Dada huyu mwanzo mwisho alikuwa akitabasamu
 Hope Makoko katika moja ya pozz zake nyingi alizozionyesha
 Mwanamke kuvaa, na hasa ukiwa na hivi kama huyu aonekanavyo
 Wamama wa pamoja,utazani mabinti wa miaka 30,siri ya mafanikio ni kujijari
 Wafanyakazi wenzake na Mr Matovero aliokuwa akifanyanao kabla hajahama Bukoba nao walijumuika kumuaga
 Kaka mkubwa, Ernest Nyambo,akiwashukuru wageni waalikwa kwa muda mfupi wameitikia wito wa kuwaaga Mr & Mrs Matovero.
 ikafika wakati wa kuwapa mkono wa kwaheri, watu walipendeza si mchezo
 Kaka mkubwa akisakata mayenu na dada Asimwe
 Watu walikaa hivi
 Chui na London(Dada Salome)katibu wa pamoja group, anafanya kazi kubwa katika umoja huu
 MENU...... kitu cha Hawa Hassan
 Hapa ni kuku mmoja anakatwa vipannde vitatu
 Maua Daftari, mmmmm
 mtu mzima Mc Jerry
Mama Mainda akisakata rumba