Thursday 13 March 2014

SITA AIBUKA KIDEDEA KWA KURA 487 KATIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KUDUMU BUNGE LA KATIBA


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Hashim Rungwe akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa akiweka karatasi ya Kura yake ya Kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wakipiga Kura Kwa ajili ya Nafasi Ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Iliyokuwa Ikiwaniwa na Bw. Edward Lowasa na Bw. Hashim Rungwe leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa Kujitengemea, Hashim Rungwe. 

Sitta ameibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika leo jioni mjini Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda, Mh Ameir Pandu Kificho, amekabidhi madaraka hayo kwa mwenyekiti mpya Samuel Sitta baada ya kumaliza rasmi muda wake wa kuliendesha bunge hilo leo. 

Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiye mshindi wa kuanza kupambana na misukosuko ya bunge hilo ambalo kwa sasa litaanza kuendeshwa kwa kanuni.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wasira akiwa na Mjumbe mwenzie wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka wakati zoezi la upigaji kura likiendelea Leo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment