Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakiimba wimbo wa Taifa kabala ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya wa Tanzania Bara walioapishwa leo wakiwa katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo cha kuzingatia maadili ya viongozi wa umma katika kutekeleza majukumu yao leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini hati za viapo vya maadili ya viongozi wa umma mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.Picha/Eleuteri Mangi na Aron Msigwa.
Na Jacquiline Mrisho- Dar es salaam.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.
Rais Dkt. Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa aliowateua Machi 13 mwaka huu ambapo amewaagiza washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaondoa watumishi hewa.
“Nimewapa siku 15 kuanzia leo mkashirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri zenu kuwatoa wafanyakazi hewa, nikigundua kuwa bado kuna wafanyakazi hewa, Mkurugenzi husika atafukuzwa kazi na atapelekwa mahakamani”,
Na kusisitiza “Nimeamua kuwachagua nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika Mikoa yenu, nawaomba mkatimize majukumu yenu bila kuogopa” alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amesikitishwa na utafiti wa watumishi uliofanywa katika Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo imegundulika watumishi 202 wanalipwa mishahara hewa.
Wakati wa utafiti huo, zaidi ya watumishi 26,900 walioko katika Halmashauri 14 za Mikoa hiyo, watumishi 3,320 hawakuwepo kazini kwa sababu mbalimbali.
Kwa mantiki hiyo, ukichukua utafiti huo wa Mikoa miwili ni dhahiri Serikali inapoteza mapato mengi kwa kulipa mishahara ya watumishi hewa nchi nzima.
Vivyo hivyo, Mhe. Dkt. Magufuli amewasisitiza Wakuu wote wa Mikoa wakasimamie ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao.
Naye Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri zote nchini wajiandae kupokea na kuzipangia matumizi shilingi milioni 50 za kila Kijiji zilizoahidiwa wakati wa kampeni kwa lengo la kuboresha na kuimarisha shughuli za maendeleo.