Wednesday 17 February 2016

KARIBU CHILDREN'S CORNER KWA MAHITAJI YA NGUO NA VIFAA VYA WATOTO,BARABARA YA KASHAI BUKOBA.

Ni duka la nguo za  watoto na vifaa mbalimbali vya watoto,(CHILDREN'S CORNER) ni duka kubwa la kisasa lipo barabara ya Kashai mkabala na shule ya msingi Tumaini, unapofika katika duka hilo utapata kila kitu kinachomhusu mwanao.
Duka hilo lipo kwenye jengo zuri,wana eneo kubwa hata kwa wale wanaokuja na magari,ipo parking ya kutosha.
Bei ni nafuu sana.
Kabati kwa ajili ya nguo za watoto.

Baiskeri za watoto zinapatikana kwa bei nafuu.Fika barabara ya Kashai karibu na shule ya msingi Tumaini.Kwa maelezo zaidi piga simu0757 242657.

Tuesday 16 February 2016

KWA TIKETI YA NDEGE YA HARAKA NA BEI NAFUU WAONE KENCAN TRAVEL AGENCY BUKOBA.

 Kencan Travel Agency ni wakala wa kuuza tiketi za ndege kwa ajili ya kusafiri ndani ya nchi na nje ya nchi, kwa mawasiliano piga simu namba 0762 257607,ofisi ipo barabara ya hospital ya Hindu Bukoba.
 Barabara ya Hindu Hospital.
 Wakala wa kuuza tiketi za ndege Bukoba.
Utakutana na dada mwenye tabasamu la kumtoa nyoka pangoni, Karibuni.

KATIKA KUMBUKUMBU ZETU,BEN MULOKOZI ATEMBELEA HOSPITAL YA NDOLAGE BUKOBA MJINI KUMPA POLE MAMA YAKE MZAZI, WAGONJWA WOTE KATIKA WODI WAPEWA MKWANJA.

Ni kawaida kumjulia hali mgojwa na kwenda kumpa pole pale anapokuwa hospital, Takriban miaka miwili iliyopita mama mzazi wa mfanyabiashara Ben Mulokozi alitokea Dar na kuja kumuona mama yake mzazi alie kuwa anaumwa na amelazwa katika hospital ya Ndolage ya Bukoba mjini inayomilikiwa na kanisa la kkkt,Bw Ben baada ya kufika hospital alimjulia hali mama yake na baada ya hapo alipita kila kitanda cha mgonjwa kumjulia hali na kujipatia pesa taslimu kwa ajili ya mlo wa siku mbili, hakika tukio hilo liliwapafaraja wagojwa na kufarijika sana na kuombewa dua nyingi,Ndugu msomaji leo  tarehe 16-02-2016 mmiliki wa mtandandao huu nimepita katika hospital hiyo kumuona mgonjwa, kwa bahati nzuri nikakutana na mmoja mwa wagonjwa aliekuwa kalazwa kipindi hicho,lakini leo nae anamuuguza ndugu yake,mara baada ya kuniona akaniuleza kwa kihaya (omushaija ayatuale amaela abayo, omushule muno) YULE BW ALIETUPA PESA KIPINDI KILE YUPO, MSALIMIE SANA. Kwa kweli binafsi kuna kitu nikajifunza hapa kuwa WEMA HAUOZI,ni miaka miwili sasa imepita tangu afanye wema huo, lakini leo mtu anakumbuka.Hakika nimejifunza kitu.SWALI WEWE UMESAIDIA WANGAPI KATIKA NEEMA ULIZOJALIWA NA MWENYEZI MUNGU, Asanteeni.
Ben akiwa na mama yake hospital.
Hata wale waliokutwa kwenye bench wakisubiri kumuona daktari walipewa pesa ya mlo wa siku hiyo.
Ni wadau waliofika kumuona mgojwa wakiwa na Bw Ben aliesimama katikati.
Wakati muafaka ukafika wa kufungua .
Wagojwa wakitembelewa.
Wasibamu ota.
Mama ugua pole.
Zoezi la kupa mlo wa siku mbili likiendelea .
Picha ya pamoja.
Safari ya kurejea Dar.

Monday 15 February 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA VITANDA MAGODORO NA MASHUKA KUTOKA MSD



Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipokea mashuka magodolo pamoja na vitanda kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD),Laurean Rugambwa Bwanakunu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na wandishi wa habari juu ya kupokea vitanda magodoro na mashuka kutoka Bohari ya Dawa (MSD) leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaidia kufagia,leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaidi kuondoa vifaa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Dk. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.
Magodoro yakishushwa
Mafundi wakifunga vitanda
Wagonjwa wakiwa katika wodi ya wazazi.