Thursday 20 November 2014

TANGAZO LA RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU LEONARD MTENSA.

MWENYEKITI KAMATI YA MAZISHI YA MAREHEMU LEONARD MTENSA ANAWATANGAZIA RAIBA YA MAZISHI KAMA IFUATAVYO; TAREHE 21-11-1014 SIKU YA IJUMAA  SAA TISA ALASIRI MWILI WA MAREHEMU UTATOLEWA HOSPITALI YA MKOA WA KAGERA NA KUPELEKWA NYUMBANI KWAKE KYAKAILABWA BUKOBA MANISPAA. NA TAREHE 22-11-2014 JUMAMOSI NDIO SIKU YA MAZISHI. RATIBA ITAANZA KUANZIA SAA SITA MCHANA, CHAKULA NA  IBADA YA MAZISHI.KWA WALE WOTE WENYE MAGARI WANAOBWA  SIKU YA TAREHE 21-11-2014 IJUMAA WAFIKE HOSPITALI YA MKOA WA KAGERA KWA AJILI YA KUUNGANA KWENYE MSAFARA WA KUPELEKA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWAKE KYAKAILABWA. ASANTENI.

Tuesday 18 November 2014

HAFRA FUPI YA UFUNGUZI WA MWEYANJARE BAR & SNACK NYAKATO MWISHO WA RAMI BUKOBA.

 Katika hali ya kusogeza huduma bora kwa watumiaji na walaji,Mkurugenzi wa Mweyanjare Bar & Snack Bw Rwehumbiza na Bi Happiness Rwehumbiza wamewekeza katika  eneo la Nyakato mwisho wa Rami na kufungua Bar & Snack kwa ajiri ya kusogeza karibu huduma bora ambazo wananchi wengi wamekuwa wakiamini huduma bora zinapatikana maeneo ya mijini tu,kitu ambacho Bw  Rwehumbiza ameamua kuonyesha kuwa hiyo dhana si sahihi popote huduma bora zinaweza kupatikana inategemea ni kwa namna gani mtoa huduma amejipanga.Mweyanjare Bar & Snack imefunguliwa maeneo ya Nyakato mwisho wa rami barabara inayokwenda Kashozi Bugabo,Unapokuwa umefika Kata ya Buhembe unaendelea na barabara inayokwenda Nyakato sekondari mwisho wa rami . Ukizingatia Manispaa ya Bukoba inazidi kupanuka , na matawi ya vyuo vikuu kuongezeka,
 Utajipatia chips na nyama choma.
 Karibu sana.
 Eneo la Counter.
 Eneo la ndani.
 Vinywaji vya aina zote vinapatikana.
 Mkurugenzi Bw  Rwehumbiza.
 Sehemu ya store.
 Mama na Baba ni kusaidiana.Mr & Mrs Rwehumbiza wakiwajibika Mweyanjare Bar & Snack karibuni kwa raha mustarehee.
 Wapo wataalam wa kuchoma nyama , kuku, mbuzi, nk.
 Vitu mchanganyiko vinapatikana.
 Mrs Happiness Rwehumbiza ambae ndio meneja mkuu akiwajibika kwa vitendo.
 Eneo hilo limepakana na chuo cha JOKUKO na ni eneo zuri tulivu , salama na huduma za uhakika.
 Watu kwa raha zao.
 Cheers.
 Hakika HAPA HATOKI MTU.
 Mchoma nyama Bw Benjamin akiwajibika.
 Mwendo wa mbilimbili.
 Serengeti kila kona wapo.
Hakika watembelee uone huduma zao. KARIBUNI WOTE.

Monday 17 November 2014

NI MIAKA SABA SASA TANGU UTUTOKE MAMA YETU MPENZI OMUGENZI MA AULELIA KOBULUNGO MUGANDA,MISA YA SHUKRANI YAFANYIKA KASTAMU BUKOBA MJINI.

 Ni Picha ya marehemu Ma Aulelia Kobulungo Muganda wakati wa uhai wake, imefanyika misa ya shukrani kwa ajiri ya kumshukuru mungu na kumuombea marehemu, Ibada ya misa imefanyika nyumbani kwa marehemu Kastam Bukoba Mjini na kuudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki,Wakati huo pia Ibada ya misa ya shukrani imefanyika jijini Dar nyumbani kwa mtoto wa marehemu James Rugemarila maeneo ya Makongo Dar.
 Mzee Robert Bahati na wazee wengine wakati wa ibada ya misa ya shukrani.
 Mama Victor (kushoto) akiwa katika Ibada.
 Kwaya ya Mt Telesia ikitumbuiza wakati wa Ibada.
 Bw Rahim Kabyemela akiwa na Bi Tunu kuhakikisha shughuri zote zinafanikiwa.
 Chakula Time.
 Mama Achi ndio alisababisha watu wakashibaaaa.
 Padri akitoa neno la bwana kwa kondoo wake.
 Mwanga wa milele umwangazie ehe bwana Ma Aulelia Kobulungo Muganda.
 Mzee kijana huyo....
 Mzee Robert Bahati akitoa neno la shukrani  kwa niaba ya familia na kwa niaba ya mzee James Rugemarila .
 Wakati wa ngoma.
 Windhock ndio ilikuwa mpango mzima..
 Kila mmoja ni kinywaji cha Windhock , hapana chezea kampuni ya Mabibo Wine chini ya mkurugenzi wake Mama James Rugemalira.
 Windhock ikawafanya wachangamke zaidi.
 Bojo Windhock nenura ushaga ensenene,chonka Ta James Rugemalirila yakolaaa.
 Tunu akifurahi na camera yetu.
 Wanafamilia picha ya ukumbusho.
 Picha ya pamoja Wanafamilia.

Pumzika kwa amani  Ma Aulelia Kobulungo Muganda.