Wednesday 22 October 2014

MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA VIJIJINI JASON RWEIKIZA AZIDI KUKATA ANGA KWA CHOPA KUCHANGIA MAABARA KATA YA KANYANGEREKO NA KEMONDO .


 Kikundi cha ngoma kata ya Kanyangereko Maruku wakimsubiri kumpokea Mbunge wao.
 Mh Dezi Diwani wa kata ya Kanyangereko.
 Mh Mbunge akiwasili eneo la mkutano.
 Mh Amida Adamu Diwani viti maalum.

 Mh Mbunge katika kata ya Kanyangareko amechangia kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajiri ya Maabara.
 Wananchi walitoa zawadi mbalimbali kwa mh mbunge Jason Rweikiza.
 Wananchi wa kata ya Kemondo.
 Waitu mwakoloaaa
Chopa inaendelea kuchanja anga kata zote 29 za jimbo.

Tuesday 21 October 2014

MBUNGE WA BUKOBA VIJIJINI JASON RWEIKIZA AFANYA MIKUTANO 5 KWA SIKU JIMBONI MWAKEKWA KUTUMIA HELKOPTA. ACHANGIA MILLIONI 37 YA UJENZI WA MAABARA NA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KATA HIZO TANO.



Mh.Mbunge wa Jimbo la Bukoba VijijiniJason Rweikiza ameendelea na Ziara katika Jimbo lake lenye kata 39 kuunga mkono tamko la Rais Jakaya Mrisho Kikwete  la kujenga Maabara katika kila Kata kwa ajili ya Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi. Mh. Rweikiza anaendesha Mwenyewe helkopta akisaidiana na Rubani mwenzake amesema kutokana na Muda kubana imebidi atumie usafiri wa Helkopta ili aweze kukimbizana na muda wa kufanya kazi za Wananchi wa Jimbo lake. Amewaomba Wananchi kuunga mkono jitihada za Rais Kikwete kuchangia ujenzi wa Maabara kwa ajili ya Wanafunzi. Mbali na kuchangi mambo mengine ya Maendelea kila Kata Mh. Rweikiza anachangia kiasi cha Milioni tatu katika Kata 39 kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara, Pia amewataka Wananchi kuunga mkono na kuipigia kura ya ndio Rasimu ya Katiba wakati wa kura za maoni ya Wananchi.
Katika Kata tano za Katoma, Karabagaine, Maruku, Kanyagereko na Kemondo amechangia kiasi cha Millioni 37,750,000/= kwa ajili ya Maabara na Miradi Mingine.

Mh.Mbunge wa Jimbo la Bukoba VijijiniJason Rweikizaakisalimiana na Wanachi Bukba Vijijini wakati wa Ziara yake inayoendelea kwa sasa.

viongozi wakisaini kwenye vitabu vya kumbukumbu

Wananchi wakisogelea Mwewe' Helkopta aliyokuja nayo Mbunge wao Jason Rweikiza.







Mr. Jamal Kalumuna akichukua kumbukumbu za Video

Wananchi wakiwa makini kumsikiliza Mh. Mbunge Rweikiza






Baadhi ya Wananchi wakiteta jambo.





Mbunge Jason Rweikiza wa Jimbo la Bukoba Vijijini (kulia) akisalimiana na baadhi ya Viongozi Kijijini Jimboni Mwake.