Manispaa ya Bukoba imeibuka kidedea katika bonanza kabambe kwa wanafunzi wa shule za msingi lililoandaliwa na shirika lisilo la serikali la Jambo Bukoba linaloendeshwa na kusimamiwa na Bw Clement Mulokozi mwenye asili ya Kitanzani na kijerumani,Bonanza kubwa lililoshirikisha timu nane kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera katika michezo tofauti lilifanyika katika viwanja vya Gymkana Manispaa ya Bukoba, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw John Mongella aliewakirishwa na Afisa elimu Mkoa Kagera Bw Frolian Kimoro.
Ni baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakiwa mbele ya jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kwa ajili ya kuanza maandamano kuelekea viwanja vya Gymkana Bukoba.
Wapiga picha kutoka Ujerumani wakichukua matukio.
Jambo Bukoba ni shirika lisilo la kiserikali linalokuza vipaji vya watoto na kusaidia mambo mbalimbali katika elimu, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya michezo, kujenga madarasa na kusaidia madawati kwa ajili ya watoto waweza kusoma katika mazingira mazuri.
Wanafunzi wakiwa wamependeza na jezi zilizotolewa na Jambo Bukoba.
Maandamano makubwa.
Mwl Lobozi Mc wa shughuli nzima.
Watu wakiwa kazini.
Waalimu wa shule tofauti.
Kushoto ni Bw Clement Mulokozi Mkurugenzi wa Jambo Bukoba akiwa na Bw Gonzaga meneja wa Jambo Bukoba Mkoani Kagera, Bw Clement Mulokozi ni mzaliwa wa Ishozi na mama yake ni Mjerumani, na kwa sasa anaishi nchini ujerumani.
Wakipokea maandamano.
Inapendeza sana.
Bw Gonzaga meneja wa Jambo Bukoba .
Mavalontia kutoka Ujerumani wanaosaidia katika shule tofauti wakijitambulisha.
Afisa michezo wa Mkoa wa Kagera akitoa neno.
Mkurugenzi wa Jambo Bukoba akitoa neno.
Balozi mstaafu nchini Ujerumani, Balozi Ngemela akieleza namna alivyoshiriki katika mchakato wa uanzishwaji wa Jambo Bukoba kipindi akiwa balozi nchini Ujerumani.
Wakinena kitu.
Mjerumani akaacha camera akanogewa muziki wa kakau band, si mchezo.
Kakau band wakitumbuiza katika Bonanza.
Meneja Gonzaga nae akacheza.
Ilikuwa ni shidaaaaa
Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Afisa elimu wa mkoa Frolian Kimoro akatoa neno.
Mhezo wa kabumbu.
Ghafla ikashuka mvua ya hatariiiiii
Tent na viti chini,bonge la mvua.
Badae hali ikawa shwari, kamati ya ufundi ya Manispaa ya Bukoba ikatabiri ushindi.
Hali ilikuwa hivi, ila kamati ya ufundi ikasema Manispaa itabeba kombe kwa michezo yote, maana ni wataalam wa kucheza majini.
Kwenye kukimbia na gunia , Manispaa nako wakaibuka kidedea.
Wanasema ni mchezo wa mpira huru,karagwe wakaibuka kidedea.
Wakati wa zawadi kila shule iliyoshiriki ilipewa milioni nne na zawadi za washindi.
Ni kifaa maalumu kinaruka angani na kupiga picha chenyewe, Bonanza lilikuwa si mchezo.
Missenye washindi wa tatu.
Muleba washindi wa pili.
Manispaa washindi wa kwanza, ilikuwa ni shidaaaa
Waalim Manispaa
Hata hawa wakaishangilia Manispaa.
Wakapewa kombe, cheti na milioni nne.
Bw Kisimba akiwa na Bw Clement.
Picha na mabingwa.
Washiriki wagine walijipatia mpira, cheti na milioni nne.
Hongera Jambo Bukoba kwa kuibua na kuendeleza michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi Mkoa wa Kagera na kusaidi kupitia michezo elimu kwa ujumla.