Friday, 26 September 2014

MCHUNGAJI ATUMIA SADAKA KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA BUKOBA

Mchungaji James

Hatahivyo mashirika, Taasisi na watu binafisi mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuchangia katika miradi mbalimbali ya Maendeleo .


Wito huo umetolewa na mmoja wa wadau wa maendeleo manispaa ya Bukoba, MCHUNGAJI KING JAMES wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara unaondelea kwa sasa.

Mchungaji JEMES  amesema kuwa amewiwa kutoa mchango huo, katika shule za manispaa zinazoendelea na ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi.

Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORAH PANGAN

Kutoka kushoto ni mkurugenzi manispaa, naibu meya Ngalinda, mchungaji James, mwenyekiti wa ccm wilaya, na afisa tarafa Abdon Khawa.



Ameongeza kuwa juhudi za serikali pekee hazitoshi katika kuwaletea wananchi maendeleo bali ni kushirikiana na wadau wote.

Akisoma risala wakati wa kupokea msaada huo mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, ADOH MAPUNDA amesema kuwa msaada huo, umetolewa kwa wakati muafaka na kutaka msaada huo kutumika kwa malengo yaliyokusudiw

ZIARA YA KINANA WILAYA YA KILINDI MKOANI TANGA




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Kwediboma wakati wa mapokezi .

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwaslimia wakazi wa Kwediboma wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kwediboma wakati wa kushiriki kujenga msingi wa kituo cha afya cha Kwediboma.

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza mawe kwenye msingi wa kituo cha afya Kwediboma.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumwaga zege kwenye msingi wa chumba cha mahabara ya Shule ya Sekondari Kibirashi wilayani Kilindi.
Wakina mama wa kimasai wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Kibirashi.
 Bendera za CCM zikipepea
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kibirashi wilaya ya Kilindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara Kibirashi,Kilindi.



Wakazi wa Kibirashi wakifuatilia yaliyojiri kwenye mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utiifu cha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

 Hivi ndivyo Kinana alivyopokelewa Kilindi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa Songe wilaya ya Kilindi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Songe wilayani Kilindi wakati wa mkutano wa hadhara.
 Umati wa watu wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Songe wilaya ya Kilindi.
 Wananchi wa Songe wakinunua nguo za CCM,Ssre za Chama Cha Mapinduzi zinazidi kupendwa siku hadi siku .
 Hili ndio Soko la Mahindi Songe.
 Wananchi wa Songe wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Songe  kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali haiwezi kufanya kila kitu hivyo hakuna ya kuongeza bidii katika kujitegemea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinunua karanga baada ya kumaliza mkutano wake kata ya Songe wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Songe.

Thursday, 25 September 2014

FASTJET YAANZA SAFARI MPYA KATI YA DAR ES SALAAM TANZANIA NA ENTEBE , UGANDA

 Captain Sagar Chavda, Muongozaji wa Ndege  Kutoka Dar es salaam kuelekea Enteber, akiwa tayari kurusha ndege katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
 Meneja wa huduma kwa wateja, Jean Uku, akizungumza na wateja wa Fastjet.
 Kushoto ni Jean Uku Commercial Manager wa Fastjet na Jimy Kibati General Manager wa Fastjet wakizindua Rasmi safari za Kwenda Entebe kutokea Dar es  salaam.
 Wageni wakikaribishwa katika Ndege ya Fastjet kutokea Dar kwenda Entebe
Timu nzima ya Fastjet Baada ya sherehe fupi za uzinduzi huo.

Ndege kati ya miji hii mikuu miwili zitaruka siku za Jumanne na Alhamisi kwa wiki za kwanza za mwezi Septemba na zinatarajiwa kuongezwa hadi mara nne kwa wiki kuanzia tarehe 29 Septemba.
Entebbe inakuwa kituo cha nne cha kimataifa kwa Fastjet ukitoa Harare, Johanesburg na Lusaka.
Mwelekeo huu mpya utapaisha ndege za moja kwa moja kati ya Entebbe na Dar es salaam kwa bei murua kabisa ukilinganisha na mashirika mengine ya ndege ambayo hutoa huduma zisizo za moja kwa moja kati ya miji hii mikubwa miwili.
Tiketi za safari hii zinapatikana kupitia www.fastjet.com kwa bei ya chini kabisa ya kuanzia Tshs. 80,000/= kwa safari moja (bila kodi).

Wednesday, 24 September 2014

RASIMU KATIBA MPYA ILIYOPENDEKEZWA YAWASILISHWA RASMI LEO KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA


 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha bunge hilo leo mjini Dodoma, wakati ikiwasilishwa Rasimu ya katiba iliyopendekezwa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalumu la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akiwasilisha Rasimu iliyopendekezwa ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya Uandishi, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, leo 24 Septemba, 2014. Kulia ni mjumbe wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson. Pichazotena Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma

Tuesday, 23 September 2014

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AMTEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO MH DAUDA ALMASUDI KALUMUNA KUMJULIA HALI.

 Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki amemtembelea Mh Dauda Almasud Kalumuna alielazwa kwa ajiri ya matibabu katika hospital ya rufaa ya Bugando.Watu mbalimbali ,ndugu, jamaa na marafiki kutoka pande mbalimbali nchini wamekuwa wakimiminika kwa wingi kwende kumjuli hali mmoja wa wanasiasa na kiongozi wa muda mrefu katika Manispaa ya Bukoba Mh Kalumuna.Kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
 Akiwa na mwanae Ashiraf kalumuna na Mdogo wake Sadick
 KULIA Partrick Pombe,Rehema Kalumuna, Erasmus George misifa, na Jose walifika kumsalimu na kumjulia hali
 Mama Mwainunu nae alifika kumjulia hali
 Kushoto ni Yusuf Elias,Jose na Jamal Kalumuna wakiwa na mgonjwa
 Balozi Kagasheki akitaniana na classmante wake akiwa kitandani,
 Katikati ni Anitha maarufu Zimbiile nae alifika kumjulia hali mgonjwa.
 Hospital ya Rufaa ya Bugando.
Tunakuombe kwa mwenyezi mungu akupe afya upone na kurudi katika hali ya kawaida.