Thursday 25 September 2014

FASTJET YAANZA SAFARI MPYA KATI YA DAR ES SALAAM TANZANIA NA ENTEBE , UGANDA

 Captain Sagar Chavda, Muongozaji wa Ndege  Kutoka Dar es salaam kuelekea Enteber, akiwa tayari kurusha ndege katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
 Meneja wa huduma kwa wateja, Jean Uku, akizungumza na wateja wa Fastjet.
 Kushoto ni Jean Uku Commercial Manager wa Fastjet na Jimy Kibati General Manager wa Fastjet wakizindua Rasmi safari za Kwenda Entebe kutokea Dar es  salaam.
 Wageni wakikaribishwa katika Ndege ya Fastjet kutokea Dar kwenda Entebe
Timu nzima ya Fastjet Baada ya sherehe fupi za uzinduzi huo.

Ndege kati ya miji hii mikuu miwili zitaruka siku za Jumanne na Alhamisi kwa wiki za kwanza za mwezi Septemba na zinatarajiwa kuongezwa hadi mara nne kwa wiki kuanzia tarehe 29 Septemba.
Entebbe inakuwa kituo cha nne cha kimataifa kwa Fastjet ukitoa Harare, Johanesburg na Lusaka.
Mwelekeo huu mpya utapaisha ndege za moja kwa moja kati ya Entebbe na Dar es salaam kwa bei murua kabisa ukilinganisha na mashirika mengine ya ndege ambayo hutoa huduma zisizo za moja kwa moja kati ya miji hii mikubwa miwili.
Tiketi za safari hii zinapatikana kupitia www.fastjet.com kwa bei ya chini kabisa ya kuanzia Tshs. 80,000/= kwa safari moja (bila kodi).

No comments:

Post a Comment