Friday 26 September 2014

MCHUNGAJI ATUMIA SADAKA KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA BUKOBA

Mchungaji James

Hatahivyo mashirika, Taasisi na watu binafisi mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuchangia katika miradi mbalimbali ya Maendeleo .


Wito huo umetolewa na mmoja wa wadau wa maendeleo manispaa ya Bukoba, MCHUNGAJI KING JAMES wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara unaondelea kwa sasa.

Mchungaji JEMES  amesema kuwa amewiwa kutoa mchango huo, katika shule za manispaa zinazoendelea na ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi.

Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORAH PANGAN

Kutoka kushoto ni mkurugenzi manispaa, naibu meya Ngalinda, mchungaji James, mwenyekiti wa ccm wilaya, na afisa tarafa Abdon Khawa.



Ameongeza kuwa juhudi za serikali pekee hazitoshi katika kuwaletea wananchi maendeleo bali ni kushirikiana na wadau wote.

Akisoma risala wakati wa kupokea msaada huo mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, ADOH MAPUNDA amesema kuwa msaada huo, umetolewa kwa wakati muafaka na kutaka msaada huo kutumika kwa malengo yaliyokusudiw

No comments:

Post a Comment