Tuesday, 3 February 2015

BEN KATARUGA AGUSWA NA KITUO CHA NUSURU YATIMA,KUJENGA BWENI MOJA,ATOA LAKI TANO CASH KWA MAHITAJI YA WATOTO.

Mfanyabiashara maarufu anaeishi jijini Dar mzaliwa wa kijiji cha Gera Bukoba vijijini  Bw Ben Kataruga ameguswa na kuwiwa kusaidia watoto yatima wa kituo Nusuru yatima kilichopo Kata Kashai Bukoba Manispaa,Mara baada ya kufika katika kituo hicho alitembezwa kujionea mazingira ya kituo hicho na kujionea namna watoto hao wanavyoishi,Kimsingi Bw Ben alibaini mazingira magumu wanayoishi watoto hao kwani mlezi na msimamizi wa kituo hicho Mama Nuru hana chanzo chochote cha kutunza watoto hao yatima.Bw Ben Kataruga akaguswa na kuamua kujenga bweni kubwa la kisasa litakalokuwa na nafasi ya kutosha na hewa ya kutosha ili watoto waweze kulala vizuri zaidi kuliko wanavyo lala kwa sasa.
Ben akipokelewa na watoto yatima alipowasili katika kituo hicho.
Watoto walifurahi walipoona wageni.
Ben akiangalia moja ya bweni lililojengwa na wafadhili.
Ben akikagua maeneo wanayolala watoto.
Akipata maelezo kutoka kwa mlezi, kwa nje ni ng'ombe waliopewa na waziri mkuu kwa ajili ya maziwa ya watoto,Kwa sasa imekuwa mzigo mkubwa kwani hawana uwezo wa kuajiri mtu wa kutunza ng'ombe hao kitu kilichosababisha afya ya mifugo kuzoofika kwa kutopata lishe bora na maana halisi ya kuwa na ng'ombe hao kupotea.
Mlezi akiendelea kutoa maelezo ya kina.
Mc Baraka akakabidhi kiai cha shilingi laki tano kilichotolewa na Bw Ben Kataruga kusaidia mahitaji mbalimbali ya watoto yatima.
Mlezi akishukuru.
Mmoja wa yatima anaetunzwa kituoni hapo,wadau tafakari na jiulize maswali mengi juu ya yatima wa umri huu na nachukua hatua.
Bw Ben aliambatana na rafiki yake Mchungaji Deo ambae nae amehaidi kusaidia.
Mara watoto wakasoma dua kuombea ugen uliofika kuwaona.
Aminaaaa.
Jamco, Bushira, Shafi ni miongoni wa waliomsindikiza Bw Ben.
Baada ya shughuli nzito msafara ukaelekea airport Bukoba, Bw Ben akiteta na Bw Hafidhu Karugila.
Jamcobukoba.blogspot.com inatoa shukra za pekee kwa Bw Ben Kataruga, kwani  baada ya blogger Jamal kumueleza habari ya kituo hiki alikubali kuwatembelea na kujionea hali halisi,Asante sana Bw Ben kwa moyo wako wa huruma na upendo, wewe ni mfano wa kuingwa na mungu akutangulie katika shughuli zako, umetambua watu wenye matatizo na mahitaji.

No comments:

Post a Comment