Friday 6 February 2015

WADAU WAZIDI KUSAIDIA KITUO CHA YATIMA CHA KASHAI.

 Ikiwa ni siku chache tu baada ya Mtandao wa Jamcobukoba na Bukoba wadau kurusha habari ya Bw Ben Kataruga kusaidia kituo cha Nusuru Yatima kwa kuwasaidia pesa  na kuwahaidi kuwajengea bweni,wadau mbalimbali wamejitokeza kwenye mitandao wakipongeza kitendo cha uungwana cha kusaidia watoto yatima,Na matunda yake yanaonekana dhairi kwa wadau kuzidi kujitokeza kusaidia,Mchungaji Deo na wadau wengine wameguswa na kuleta vyakula, mchele,sukari, mafuta ya kula, sabuni, chumvi , biskuti nk kwa ajili ya matumizi ya watoto.
 Bushira na shafi wakibeba vyakula vya watoto.
 Mchungaji Deo nae akibeba vyakula vya watoto.
 Watoto wakifurahia.
 Mfuta ya kula.
 Picha ya pamoja.
 Mlezi akipokea vyakula.
 Blogger Jamal wa mtandao huu mwenye Tshirt nyeusi akiwa na wadau.
 Ni  bibi  Prisca George Isaya  Kaimu mwenyekiti wa kituo cha Nusuru yatima kashai akitoa shukrani kwa Mchungaji Deo na ujumbe aliofuatana nao kwa msaada wa vyakula walivyoleta.
Wadau tunawashukuru, wazidi kujitokeza kusaidia watoto hao yatima.

No comments:

Post a Comment