Wednesday, 3 December 2014

NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB KUFUNGULIWA MULEBA TAREHE 5-12-2014,WASANII MAARUFU KUWEPO, MRISHO MPOTO, ELIZABERT LULU,JACKLINE WOLPER,DUDE NA BENDI NZIMA YA MUUMIN JUMA.

 Ni eneo la nje la hotel ya kisasa itakayofunguliwa 5-12-2014,sherehe ya ufunguzi itaanza saa nne asubuhi kwa ibada maalumu ya ufunguzi mpaka saa sita mchana, Baada ya hapo yatakuwepo mapumziko na ratiba itaanza tena saa 12.00 jioni mpaka majogoo.
 Maeneo ya NALPHIN HOTEL INAYOFUNGULIWA 5-12-2014.
Maandalizi yakiendelea kwa ajili ya ufunguzi 5-12-2014.
 Maeneo ya nje ya hotel.
 Chumba cha single.
 Vyumba vya double.
 Maeneo ya vyumba.
 Eneo la tiketi Night club.
 Njia ya kuingia Night club.
 Night club mandalizi ya ufunguzi yakiendelea.
 Kitu cha uhakika.
 Viti vitakavyotumika eneo la Night club.
 Eneo la Night club.
 Eneo la ukumbi wa kisasa wakiwa katika maandalizi ya ufunguzi.
 Majiko ya kisasa ya kuchoma nyama yakiwasili kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa hotel.
 Kushoto ni meneja wa Hotel akiwa na Mkurugenzi na mmiliki wa hotel.
 Katikati ni Mkurugenzi na mmilikiwa  NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB akiwa katika mahojiano na mmiliki wa mtandao wa Jamcobukoba.blogspot.com
 Sehemu ya Bar ndani ya Night club wakimalizia marekebisho baadhi.
 Mtambo mzito.
 Dj Max akiwa anafungwa vifaa vipya na vya kisasa vitakavyotumika katika Night club.
Hi si ya kukosa tarehe 5-12-2014 karibuni sana.

Monday, 1 December 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, KITAIFA MKOANI NJOMBE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika  Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe , Desemba 2014. Picha na OMR
 
 kuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, akijumuika na wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Kanisa la KKKT, wakati wakitoa burudani yenye ujumbe kuhusu maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi Duniani. Picha na OMR
 
 Baadhi ya wandamani wakipita mbele ya jukwaa kuu na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu siku ya Ukimwi Duniani wakati wa sherehe hizo zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe  Desemba 1, 2014. Picha na OMR
 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika uwanja wa Sabasaba baada ya kuhutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa huo Mkoani Njombe. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi wakati akiondoka uwanjani hapo baada ya kuhutubia katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Njombe. Picha na OMR

GEDIOSE MUKULASI NA DORICE MBOYERWA WAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA BUKOBA.


 Ni siku ya historia katika maisha yao ya hapa duniani Bw  Gediose Mukulasi na Bi Dorice Mboyerwa,kwani wameingia katika mkataba ambao hakuna miongoni mwao anaweza kuuvunja mpaka hapo mmoja wao kwa mapenzi ya mungu anaweza kukutwa na mauti.Ilikuwa ni furaha, nderemo na vifijo katika kanisa la Kikatoliki Cathedral Bukoba mjini  mbele ya waumini na hakimu wa kiroho walipotamka na kukubaliana kuishi pamoja milele.Baada ya hapo sherehe kubwa ya kuwapongeza ilifanyika katika ukumbi wa Lake hotel iliyohudhuriwa na wageni zaidi ya mia sita.Bw harusi na bi harusi ambao wanaishi nchini Marekani.
 Mbele ya hakimu wa kiroho ,wakiweka agano la kuishi milele.
 Baada ya ndoa.
 Pendeza sanaaaaa.
 Picha ya pamoja.
 Beach.
 Wazazi wakiingia ukumbini.
 Bw NA Bi Mboyerwa wazazi wa bi harusi.
 Mzee Paul Bashereka.
 Ukumbi wa Lake hotel .
 Kifamilia zaidi.
 Mzee Mugisha akiwa na mwanae.
 Wapambe nao wakiingia ukumbini.
 Twende mke wangu.
 Mwenyekiti akifungua sherehe.
 Maharusi wakiingia ukumbini.
 BONGE LA KEKI iliyotengenezwa na mama Simeo.
 Tunakata hii keki, wote wenye husda, fitina na roho mbaya  washindwe na kulegea kwa jina la yesu.
  KARIBU KEKI MKE WANGU.
 Keki kwa wazazi wa Bw HARUSI.
 Keki kwa wazazi wa Bi harusi.
 Keki kwa wanakamati.
 Keki kwa wanafamilia.
 Kushoto, Bi Paskazia Barongo akiwa na Murungi Kichwabuta.
 Mama Matungwa mpambaji akifurahi na camera yetu.
 Dada wa Bw Harusi.
 Bw Wilson akiwa na mkewe.
 Chui na Landon akiwa na Devota ndani ya nyumba.
 Mandhari ya ukumbi,Mama Adventina matungwa ndio aliepamba.
 Hapana chezea wa mama wanaweza.
 Mr & Mrs Dr Mboyerwa wakitoa zawadi kwa maharusi.
 Bibi wa  bi Harusi akitoa zawadi kwa Bw harusi.
 Wanakamati.
 Kamati ya maandalizi.
 Nshomile family msanii akifanya yake.
 Chakula time.
 Naomba nikupe kidogooooo.
 Naomba nikurishe mpenzi.
 Mzee Paul Bashereka akipata msosi.
 Mambo ya ngoma.
 Bw Harusi akitoa shukrani kwa wote walioshiriki kuandaa harusi yao.
 Mpenzi tumetimiza ahadi yetu.
 Bw Kahabuka akionyesha uwezo wake katika kusakata rumba.
 WAGENI WAALIKWA WAKISEREBUKA,Jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maisha mema ya ndoa.