Saturday 17 December 2016

Bi SOPHIA HASSAN ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA,WATOTO WAMFANYIA SUPRISE YA GARI...

Ilikuwa na mshangoa mkubwa na machozi ya furaha kumtoka Bi sophia Hassan pale mmoja wa watoto wake nnealipotamka maneno haya, Mama tunakupenda sana, umetulea, umetosomesha ukiwa peke yako, wewe ndio ulikuwa baba, wewe ndio ulikuwa mama hatuna cha kukulipa zaidi ya kusema Asante mama yetu mpenzi naomba upokee funguo hizi za gari , na gari ni hilo hapo mbele yako naomba nikukabidhi....Hakika mama aliduwaa na kuganda kwa sekunde kadhaa, ilikuwa ni mshangao kwa wageni waalikwa katika ukumbi wa Nalphin Hotel iliyoko  Mkoa wa Kagera wilaya ya Muleba,Bi Sophia Hassan ambae amitimiza miaka 60 ya kuzaliwa na miaka 37 ya utumishi wa umma uliotukuka katika idara ya afya, Bi Sophia  katika hotuba yake anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumjalia umri wa kuishi miaka 60, na kutumikia Taifa kwa miaka 37, lakini kikubwa ameweza kusomesha wanae, mwisho anashukuru wageni walikwa , ndugu na jamaa wote kwa kufika , kwa kugusa maisha yake na alimaliza kwa kuwaomba ushirikiano katika maisha baada ya kustaafu.
Bi Sophia Hassan  muonekano wake mapema kabla ya kuingia ukumbini.
Kama kasichana hivi, miaka 60 hapo.
Eneo la kupigia picha ukumbini.
Wajukuu.
Mc akiendesha shughuli.
Bi Sophia akiingia ukumbini.
Asanteni kwa kuja....
Ilikuwa poa sana.
Muonekano wa waalikwa.
Watoto nao wakaingia ukumbini.
Ilikuwa ni shidaaa, wimbo wa nikulipe nini mama...
Asante farida, katika mpasho Khadija kopa cha mtoto..
Farida ni shidaaaa.
Sherehe ikafunguliwa kwa dua.
Bw Tele Ghama mwenyekiti wa kuratibu sherehe akatoa neno la ufunguzi.
Keki ikakatwa.
Mama mzazi wa Bi Sophia Hassan.
Mjukuu akimlisha Bibi keki.

Mama naomba upokee funguo za gari , hilo hapo mbele yako, bonge la suprise...
Dua.
Bi Sophia Hassan akatoa neno.