Friday, 30 May 2014

CAMERA YETU MKOA WA GEITA NA SENGEREMA

 Umeshawahi kupanda kivuko ..... hebu jaribu siku moja utafurahia...
 Bushira akiwa mitaa ya Geita
 Stand ya Mabasi Geita
 Hiyo ndo Geita
 Ni moja ya Hotel kubwa Mkoani Geita
 Mkoa wa Geita unakua kwa kasi kubwa sana, na watu wanawekeza vitu vikubwa
 Moja ya shule  iliyoko Mkoa wa Geita
 Ni abiria wanaotoka Mwanza wakivuka kuelekea Geita,Bukoba nk.
 Hakika Tanzania tuna Neema na maeneo mazuri ya kupendeza
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye kivuko
 Sikuweza kupata mwenyeji kunieleza msalaba huo kati jiwe unamanisha nini,ni maeneo ya sengerema
Ni muonekano wa mawe mazuri,maeneo ya Sengerema

WASHINDI WATANO SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS KUANZA KUTAFUTWA JIJINI DAR LEO


 Msimamizi wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya Pwani.
 Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza
 Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions
 Washiriki wakisoma fomu kwa makini
Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
****************************************************
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda ya Pwani Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba washiriki zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano hilo
Shindano hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya kuigiza ambalo limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi watano watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana. 
Baada ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi takribani 20 kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi moja Jijini Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye mshindi mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Vilevile Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya pamoja na hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo

Thursday, 29 May 2014

MALAIKA BAND YAPAGAWISHA WAKAAZI WA BUKOBA. WIMBO MPYA "NANI KAMA MAMA" WAKAMATA NAFASI UKUMBINI LINA'S CLUB!

Na Faustine Ruta, Bukoba
BENDI ya muziki wa dansi ya Malaika yenye masikani yake jijini Dar es salaam, Ilipagawisha wakazi wa Mkoa wa Kagera Vilivyo kwenye ziara yao katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Huku wakishuhudia sauti yenye mvuto ya mwimbaji mahiri Christian Bela na kundi zima la wanamuziki wa Malaika bendi lakini pia walipata fursa ya kuzisikia live nyimbo zao na ufundi wa wapigaji vyombo na wacheza show wakali bila kumsahau Rapa mkali Totoo ze Bingwa. “Bela aliutambulisha live kwa kuimba wimbo wake mpya unaotamba kwa sasa katika Radio, TV na Kumbi za burudani wa “Nani kama Mama”
Ziara hii baada ya kumaliza hapa Mjini Bukoba wanaelekea  Jijini Mwanza, Jiji la Miamba ya Mawe (Rock City) ambapo bendi ya Malaika itatoa burudani ya uhakika ndani ya Villa Park Resort ambapo Bela ambaye hujiita Rais wa Vijana atafanya makubwa tarehe 31, Mei 2014 siku ya Jumamosi kiingilio kikiwa ni Tsh:10,000/ = tu.
Wakazi wa Mwanza zamu yenu sasa hiyo! Hakuna kukosaaa!!
Kiti kinawaka moto ....
Waimbaji wa Kundi la Malaika wakiwasha moto ukumbini Lina's Usiku
Rapa Totoo Ze Bingwa akiimba
Muziki ndio kazi yangu ...Twende kazi wakazi wa Bukoba!!!!
Bia mpya ya Serengeti ilihusika sehemu hiyo aina Serengeti Platinum
Wapenzi na Mashabiki wa Bendi ya Malaika wakiwa tayari kwa kuburudika na Muziki huo pendwa wa Dansi hapa Nchini.
Waimbaji wa Band ya Malaika wakikamua vilivyo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Lina's Club uliopo Bukoba Mjini.
Wacheza Show wakibanjuka tuu
Hakika Malaika Band ni balaa!!!
Waimbaji wa Kundi la Malaika Band wakitoa Burudani
Dadaz wakifuatilia kwa karibu sana Burudani kutoka kwa Malaika Band kutoka jijini Dar es salaam

Marafiki: Bw. Mutensa na rafiki yake Ticha wa Leo leo wakipeana neno
....peupe na wazi wazi ....chezea Malaika Band wewe!! Dada Maua akiwa kwenye kasi mbaya!! 120!
Unachezea Muziki wa Dansi weye!!!
Kazi ipo kweli kweli!!!
Christian Bela

GARI (COSTER) LINAUZWA,PIGA SIMU 0756 818480 AU 0713 535500

 Gari aina ya Coster liko katika hali nzuri linauzwa,na huo ndio muonekano wake ulivyo, bei ni nafuu kwa mawasiliano zaidi wasiliana na muhusika kwa simu namba 0756 818480 au 0713 535500
Piga simu kwa maelezo zaidi.