Monday, 26 May 2014

PAPA FRANCIS AOMBEA UKUTA WA BETHLEHEMU.



Papa Francis akiombea ukuta wa Bethlehemu
Papa Francis ameombea ukuta wa saruji ambao Israel inajenga kulitenga eneo la ukingo wa Magharibi huko Bethlehem.
Aliweka kichwa chake juu ya juu ya ukuta huo, ambapo kumechorwa maneno" ipe uhuru Palestina".
Pande zote mbili zimekubali mwaliko.Papa ametoa mwaliko kwa Wa-Israili na Wapalestina waende Vatikani, kuomba mzozo wao umalizike.

Hapo awali Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani aliutaja mzozo kati ya Palestina na Israel kama usiokubalika huku akizitaka pande zote mbili kufanya maamuzi ya busara ili kuweka amani.
Akizungumza mjini Bethlehem ,papa Francis ametaka kubuniwa kwa taifa huru la Palestina pamoja na Israel.
Aidha alifanya maombi katika eneo ambalo Yesu anadaiwa kuzaliwa.
Akiwa katika ziara yake ya mji wa Bethlehem ,kiongozi huyo wa dini alisimama katika eneo ambalo Israel inajenga ukuta mkubwa pamoja na eneo la West bank ili kufanya maombi.
Maandishi yaliokuwa juu yake alipokuwa akiomba yalisema 'papa tunamtaka mtu atakayezungumzia kuhusu haki'.

No comments:

Post a Comment