Monday 26 May 2014

FELIX MULOKOZI FRANCE BWAHAMA MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE YA UNUNUZI WA KINANDA CHA KWAYA PAROKIA YA NGOTE MULEBA

 Bw Felix Mulokozi ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa ununuzi wa kinanda katika parokia ya Ngote, kigango cha madalena wilaya ya Muleba akizungumza na waumini na kuamasisha watu mbalimbali kuthamini na kushiriki kusaidia katika mambo ya kiroho,Bw Felix Mulokozi  alieambatana na mkewe Bi Jesca Kokushoborora na mtoto wao na kumuwakilisha Dada yao Monica France Bwahama walichangia kiasi cha milioni moja,Mh Mbunge Prof Anna Tibaijuka kupitia kwa Mgeni rasmi alichangia shilingi laki mbili na nusu,na wadau mbalimbali ambao jumla yake ilfika milioni mbili na laki nne ambayo inakidhi ununuzi wa kinanda hicho,mbali na kinanda ,yapo mahitaji ya mwalimu wa kufundisha kwaya na kutengeneza albamu ya video na mahitaji ya gharama zote ni shilingi milioni kumi. Hivyo kupitia hotuba ya mgeni rasmi awewaomba watu mbalimbali kupitia vyombo vya habari kuguswa na jambo hili na kusaidia kwaya hii hili waweze kulitangaza neno la mungu.
 Wanakwaya wakisoma risara mbele ya mgeni rasmi
 Bi Jesca(mke wa mgeni rasmi) akiwa na mtoto wao Natasha.
 Mgeni rasmi akiongea na waumini wa  Parokia ya Ngote Karambi.
 Wakati wa harambee unatoa ulichonacho
 Anaonyesha dole gumba na ni muumini wa serikali mbili
 Baada ya kufikia malengo ya kinanda wakacheza kwa raha zao, ila bado mwalimu na fedha za kurekodi video ya albamu yao,wasaidie wanakwaya hawa.
Hapa Mgeni rasmi akiteta kitu na Padre.

No comments:

Post a Comment