Thursday 29 May 2014

MALAIKA BAND YAPAGAWISHA WAKAAZI WA BUKOBA. WIMBO MPYA "NANI KAMA MAMA" WAKAMATA NAFASI UKUMBINI LINA'S CLUB!

Na Faustine Ruta, Bukoba
BENDI ya muziki wa dansi ya Malaika yenye masikani yake jijini Dar es salaam, Ilipagawisha wakazi wa Mkoa wa Kagera Vilivyo kwenye ziara yao katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Huku wakishuhudia sauti yenye mvuto ya mwimbaji mahiri Christian Bela na kundi zima la wanamuziki wa Malaika bendi lakini pia walipata fursa ya kuzisikia live nyimbo zao na ufundi wa wapigaji vyombo na wacheza show wakali bila kumsahau Rapa mkali Totoo ze Bingwa. “Bela aliutambulisha live kwa kuimba wimbo wake mpya unaotamba kwa sasa katika Radio, TV na Kumbi za burudani wa “Nani kama Mama”
Ziara hii baada ya kumaliza hapa Mjini Bukoba wanaelekea  Jijini Mwanza, Jiji la Miamba ya Mawe (Rock City) ambapo bendi ya Malaika itatoa burudani ya uhakika ndani ya Villa Park Resort ambapo Bela ambaye hujiita Rais wa Vijana atafanya makubwa tarehe 31, Mei 2014 siku ya Jumamosi kiingilio kikiwa ni Tsh:10,000/ = tu.
Wakazi wa Mwanza zamu yenu sasa hiyo! Hakuna kukosaaa!!
Kiti kinawaka moto ....
Waimbaji wa Kundi la Malaika wakiwasha moto ukumbini Lina's Usiku
Rapa Totoo Ze Bingwa akiimba
Muziki ndio kazi yangu ...Twende kazi wakazi wa Bukoba!!!!
Bia mpya ya Serengeti ilihusika sehemu hiyo aina Serengeti Platinum
Wapenzi na Mashabiki wa Bendi ya Malaika wakiwa tayari kwa kuburudika na Muziki huo pendwa wa Dansi hapa Nchini.
Waimbaji wa Band ya Malaika wakikamua vilivyo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Lina's Club uliopo Bukoba Mjini.
Wacheza Show wakibanjuka tuu
Hakika Malaika Band ni balaa!!!
Waimbaji wa Kundi la Malaika Band wakitoa Burudani
Dadaz wakifuatilia kwa karibu sana Burudani kutoka kwa Malaika Band kutoka jijini Dar es salaam

Marafiki: Bw. Mutensa na rafiki yake Ticha wa Leo leo wakipeana neno
....peupe na wazi wazi ....chezea Malaika Band wewe!! Dada Maua akiwa kwenye kasi mbaya!! 120!
Unachezea Muziki wa Dansi weye!!!
Kazi ipo kweli kweli!!!
Christian Bela

No comments:

Post a Comment