Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri
wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi
alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu, Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri
wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi
alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu, Dar Es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri wa Uchumi, Biashara na
Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo naye Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri
wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi
(wa tatu kushoto, mbele) na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Uchukuzi
Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr
Mary Nagu (wa pili kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah
Kigoda (wa pili kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome
Sijaona (wa kwanza kushoto) alipokutana na kufanya mazungumzo naye
Ikulu, Dar Es Salaam,
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
.
Japan yatangaza sera mpya kwa Tanzania
·
Sasa Tanzania kuwa nchi lengwa
ya Japan
·
Japan itasaidia Tanzania kuwa
kitovu cha uwekezaji katika Afrika
·
Kushiriki maboresho Reli ya
Kati
·
Kusaidia kupanua na kuboresha
Bandari ya Dar Es Salaam
·
Viwanda vya Japan kujengwa
nchini kikiwemo cha kutengeneza pikipiki za Honda
·
Ni matokeo ya Ziara ya Rais
Kikwete Japan
JAPAN
imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambako nchi hiyo
itaifanya Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan na kuiwezesha kuwa kitovu cha
biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika
na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.
Uamuzi
huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa
Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi
hiyo Juni, mwaka huu, 2013.
Uamuzi
na msimamo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na
Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu
Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kwa
upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na
Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Dkt.
Harrison Mwakyembe.
Waziri
Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia
mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi
lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika
Afrika kwa jumla.
Waziri
Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa
Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya
Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema
kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya
uboreshaji wa Reli hiyo.
Aidha,
Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji
wa Bandari ya Dar Es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.
Waziri
Motegi amesema kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano
katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la
wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na
wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika
kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.
Waziri pia amesema kuwa
moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa
sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika
viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.
Kwa
kuanzia amesema kuwa makampuni mawili ya Honda na Panasonic yamekubali kujenga
viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa
nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.
“Huu
ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania
kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan
katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana
katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania,” Mheshimiwa Motegi amemwambia
Rais Kikwete.
Waziri
huyo pia amesema kuwa baadhi ya makampuni ya Japan yana mipango ya kuwekeza
katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa
hapa nchini.
Wakati
wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza
zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani
ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.
Uamuzi
huo wa Japan na ziara ya Mheshimiwa Motegi inakuja wiki na miezi michache baada
ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya
Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania
zinavyokubalika duniani.
Ends
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10
Agosti, 2013