Thursday, 8 August 2013

MWANDISHI NA MTANGAZAJI WA ITV RENATUS MUTABUZI AZUA TAFRANI SOKO KUU BUKOBA,PHILBERT KATABAZI NYERERE WAFANYABIASHARA WAMUAMURU KUONDOKA MARA MOJA MAENEO YA SOKO BAADA YA KUONEKANA MAPEMA DUKANI KWAKE NA MWANDISHI WA ITV


 Ndugu philbert nyerere ambae wafanyabiashara wa soko kuu walimtaka kuondoka maeneo ya soko ,wafanyabiashara waliokuwa na hasira walimtakaatoke maeneo hayo baada ya mmoja wa wafanyabiashara hao kusema mwandishi wa ITV Renatus mutabuzi kabla ya kuja soko kuu alionekana akiwa dukani kwa ndugu philbert nyerere maeneo ya stand ya mabasi bukoba,hivyo wafanyabiashara wakaonyesha kuwa mwandishi wa ITV habari atakazotoa hazitakuwa na ukweli wowote.wafanyabiashara wa soko kuu walimueleza mwandishi wa habari kuwa swala lao liko mahakamani kwa hiyo kama anahitaji maelezo kuhusu soko ni vizuri akaenda mahakamani ataeleweshwa zaidi
 mtendaji wa kata akiwa na viongozi wa wafanyashara soko kuu na mwandishi wa habari wa ITV Renatus mutabuzi ambae aliingia soko kuu na kuendelea kufanya mahojiano na wafanyabiashara bila kutoa taarifa katika ofisi za soko,kitu ambacho kilisababisha mtafaruku mkubwa baada ya wafanyabiashara kumtaka kutoa maelezo na hali hiyo kupelekee kufika katika ofisi kwa mazungumzo ya kina

                                     mabishano yakiendelea katika ofisi za soko

                                                            watu wakaonyesha hasira zao
 imekuaje utokee kwa nyerere ndio uje rekodi habari,tutakuamini vipi kwamba utatoa habari ya ukweli,watu walihoji,
                                   mtendaji akamuhoji mwandishi ilikuaje ukaingia kurekodi bila kutoa taarifa?
 mwandishi akajieleza, yeye katumwa na serikali,watu wakahoji serikali gani na nani kamtuma wakati swala liko mahakamani?
                                                    ikabidi wazee wa busara waingilie na kushauri
 nje ya ofisi ya mtendaji wafanyabiashara ikawa zogo,wengine wakitaka asalimishe tape aliyorekodi hawali wajirizishe kilichomo, na wengine wakitaka atoke sokoni


                                                          wakamtaka mwandishi atoke sokoni        
                                                                       ilikuwa kila mmoja kivyake
 mwenyekiti wa wafanyabiashara soko kuu ndugu Hassan akiwahutubia wenzake,na kuwaeleza maamuzi waliyofikia na mwandishi wa habari
                                            mkurugenzi wa vision redio nae akafika kutaka kujua kulikoni
 mwandishi wa ITV mwenye T,shirt ya mistari akiwa nje ya ofisi ya afisa mtendaji alimtaka atoke kwenye eneo la soko ili kutuliza kelele na mabishano yaliyokuwa nje ya ofisi ya mtendaji
                    Wafanyabiashara wa soko kuu wakiwa katika hali ya kutoelewa kinachoendelea

No comments:

Post a Comment