Wednesday 7 August 2013

Angalia PICHA HUU NDO MUONEKANO WA MH.MNYIKA NA MBOWE KABLA YA KUWA WABUNGE...

                   Asikwambie mtu bwana ,ubunge ni kitu kingine,watasema sana lakini hakuna asieupenda,tumekuwa tukiona nyakati za chaguzi,wagombea wakitumia nguvu kubwa kuutafuta ubunge kuanzia kwenye uteuzi katika vyama vyao mpaka kwenye uchaguzi wa jumla kwa wananchi, wamekuwa wakijinadi na kuwaakikishia wananchi kuwaletea maendeleo na kutatua kero zao, lakini baada ya kuwa wameupata ubunge ni wachache sana wanaokumbuka ahadi zao, wengi wao uangalia masrahi yao na familia zao, wengine wanakuwa mahodari sana wa kulalamika bungeni  na kuonekana kwenye tv kupinga  na kugoma,lakini linapokuja swala la posho na masilahi binafsi hakuna anaekumbuka ufisadi,na hili limekuwea ni tatizo la wabunge wa vyama vyote,nitawaona majasiri kama siku moja watasema posho za mojawapo ya bunge kipindi chote wasichukue posho na zipelekwe kusaidia wenye matatizo,lakini wanapozungumza kwa maneno utekelezaji ziro haina maana.

No comments:

Post a Comment