Friday 24 April 2015

TEA YAKABIDHI VITABU VYA KIADA KWA SHULE MSINGI 48 ZA MIKOA YA DAR NA PWANI


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vitabu vya kiada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent vilivyotolewa na Kampuni ya Oxford University Press kwa ajili ya Shule za Msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Bagamoyo juzi. Wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa Oxford, Fatma Shangazi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Respicius Selestin. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia hafla ya ugawaji wa vitabu kwa Shule za Msingi.
Wanafunzi wa Shuleya Msingi Majengo wakisaidia kupanga vitabu.

Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe (kushoto) akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo ya Bagamoyo wakiandaa vitabu vilivyotolewa kwa shule za msingi 48 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent akizungumza katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga akizungumza katika hafla hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo akizungumza katika hafla hiyo.
Burudani ya ngoma.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jitegemee wakitumbuiza kwa ngoma za asili.
Sarakasi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo wakionyesha vipaji.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo iliyopo Bagamoyo, Munzili Feruzi akionyesha umahiri wa kuruka sarakasi wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu kwa shule za msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani iliyofanyika mjini Bagamoyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu vya kiada kwa Shule 48 za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majdi Mwanga (wa pili kushoto) akimkabidhi kitabu cha kiada mwanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo, Moza Mketo baada ya kupokea msaada wa vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya Oxford University Press kwa ajili ya Shule za Msingi 48 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Bagamoyo juzi. Kulia ni Meneja Mkuu wa Oxford, Fatma Shangazi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Respicius Selestin.

BASATA WAMPONGEZA MAYUNGA KWA KUWAKILISHA VYEMA TANZANIA



Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika. Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika katika ofisi za BASATA. Akishuhudia kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .

Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya na kumtakia kila laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika.

HABARI NJEMA KWA WANABLOGU WATANZANIA JUU UANDIKISHAJI WANACHAMA TBN

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.

SHINDANO LA TMT 2015 LAZINDULIWA RASMI LEO, MWANZA KUFUNGUA PAZIA LEO APRIL 24 2015.


Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.

Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P

Mmoja wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam

Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi wa TMT 2015, Saul Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote".
Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano hili.
Kwa kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es Salaam.

Katika kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.TMT 2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May 2015.



Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na TMT kwa mwaka 2015

Kauli Mbiu ya TMT 2015 ni Mpaka Kieleweke.

AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO MKOANI MOROGORO


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete (pichani kati) na Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda (pichani shoto) wakishuhudia askari wa jeshi la Wananchi (JWTZ) wakipiga risasi hewani kama sehemu ya heshima ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera leo,Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (mstaafu) huko kwenye makaburi ya Mlima Kola Kigurunyembe mkoani Morogoro. PICHA NA IKULU.