Thursday 29 September 2016

WATUHUMIWA WA AKAUNTI YA MAAFA KAGERA WATINGA MAHAKAMANI LEO 29-9-2016 BUKOBA.

 Watumishi watatu wa serikali  akiwemo Meneja wa CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani leo na kusomewa mashitaka mawili ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016, Watumishi waliofikishwa  mahakamani  leo ni aliekuwa katibu tawala wa mkoa Kagera  Amantus Msole, mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba kelvin Makonda, mhasibu wa mkoa kagera  Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa. Akiwasomea mashitaka  yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi wa Bukoba wakili wa serikali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili, kosa la kwanza kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana  na jina la akaunti ya  KAMATI MAAFA KAGERA yenye  no. 0152225617300, ambapo wao walifungua no. 0150225617300,shitaka la pili kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume na sheria.Hakimu mkazi wa mahakama ya Bukoba Denis  Mbelembwa alihairisha kesi hiyo mpaka kesho saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na kujiridhisha kama watuhumiwa wanastaili dhamana, na kutaka watuhumiwa warudishwe  rumande.

Wednesday 28 September 2016

SERIKALI NA KAMPUNI YA HALOTEL YATOA POLE SHILINGI 1,885,000 KWA KILA FAMILIA 17 ZILIPOTEZA NDUGU KWENYE TETEMEKO KAGERA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu amekabidhi kiasi cha shilingi  milioni 17 kwa niaba ya serikali kwa familia za marehemu waliofariki katika janga la tetemeko la ardhi liliotokea 10-9-2016 katika mkoa wa kagera na kusababisha vifo na majanga makubwa,pia kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa kiasi cha shilingi  15,045,000 kwa ajili ya pole kwa familia  zilizopoteza ndugu,kila familia imeweza kupata pole ya shilingi 1,885,000, Watu 17 walipoteza maisha wakati wa tetemeko, serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila familia na kampuni ya simu za mkononi Halotel imetoa kiasi cha shilingi 885,000 kwa kila familia.(katika picha mkuu wa mkoa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu akikabidhiwa kiasi cha milioni 15,045,000 na mkurugenzi  Bw Tran  Hieu Nghia wa Halotel akiwa na msaidizi wake  Bw  Naswiru Zuberi.)


 Ndugu wa marehemu waliofika kupokea pole.




 Halotel wakikabidhi  15, 045,000.
 Poleni kwa kupoteza ndugu.
Kushoto  ni mkurugenzi msaidizi Bw Naswiru Zuberi wa halotel Kagera, Bw Tran Hieu Nghia mkurugenzi na Bw  Johanes Julius afisa wa halotel Kagera.

ALIEKUWA KATIBU TAWALA KAGERA MBALONI NA WENZAKE.

 Aliekuwa katibu tawala  Mkoa wa Kagera Bw   Amantius Msole na wenzake wamekamatwa na polisi kufuatia agizo la rais John Mgufuli kutengua uteuzi wake na wenzake baada ya kugundulika kufungua akaunti tofauti ya Maafa ya tetemeko la ardhi mkoa wa kagera,Bw Msole, alikuwa mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Bw Steven Makonda,mhasibu wa mkoa, na meneja wa benki ya CRDB Bukoba wamekamatwa lwa ajili ya uchunguzi kufanyika kufuatia tuhuma ya kufungua akaunti itwayo Kamati Maafa Kagera kwa lengo la kujipatia fedha.(katika picha ni aliekuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Msole akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi akitolewa ofisini kwake na kurudishwa polisi baada ya upekuzi.)
 Kikazi zaidi.
Tunaendelea kumtafuta kamanda wa mkoa wa Kagera kwa habari zaidi.