Thursday 29 September 2016

WATUHUMIWA WA AKAUNTI YA MAAFA KAGERA WATINGA MAHAKAMANI LEO 29-9-2016 BUKOBA.

 Watumishi watatu wa serikali  akiwemo Meneja wa CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani leo na kusomewa mashitaka mawili ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016, Watumishi waliofikishwa  mahakamani  leo ni aliekuwa katibu tawala wa mkoa Kagera  Amantus Msole, mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba kelvin Makonda, mhasibu wa mkoa kagera  Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa. Akiwasomea mashitaka  yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi wa Bukoba wakili wa serikali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili, kosa la kwanza kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana  na jina la akaunti ya  KAMATI MAAFA KAGERA yenye  no. 0152225617300, ambapo wao walifungua no. 0150225617300,shitaka la pili kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume na sheria.Hakimu mkazi wa mahakama ya Bukoba Denis  Mbelembwa alihairisha kesi hiyo mpaka kesho saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na kujiridhisha kama watuhumiwa wanastaili dhamana, na kutaka watuhumiwa warudishwe  rumande.

No comments:

Post a Comment