Mkuu wa Mkoa wa Kagera meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 17 kwa niaba ya serikali kwa familia za marehemu waliofariki katika janga la tetemeko la ardhi liliotokea 10-9-2016 katika mkoa wa kagera na kusababisha vifo na majanga makubwa,pia kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa kiasi cha shilingi 15,045,000 kwa ajili ya pole kwa familia zilizopoteza ndugu,kila familia imeweza kupata pole ya shilingi 1,885,000, Watu 17 walipoteza maisha wakati wa tetemeko, serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila familia na kampuni ya simu za mkononi Halotel imetoa kiasi cha shilingi 885,000 kwa kila familia.(katika picha mkuu wa mkoa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu akikabidhiwa kiasi cha milioni 15,045,000 na mkurugenzi Bw Tran Hieu Nghia wa Halotel akiwa na msaidizi wake Bw Naswiru Zuberi.)
Ndugu wa marehemu waliofika kupokea pole.
Halotel wakikabidhi 15, 045,000.
Poleni kwa kupoteza ndugu.
Kushoto ni mkurugenzi msaidizi Bw Naswiru Zuberi wa halotel Kagera, Bw Tran Hieu Nghia mkurugenzi na Bw Johanes Julius afisa wa halotel Kagera.
No comments:
Post a Comment