Umati mkubwa ambao ulifika nyumbani kwa gwiji wa siasa na miongoni mwa wanasiasa wachache waliowahi kushika madaraka makubwa wakiwa na umri mdogo ,walifika kushuhudia sherehe yake ya mwisho katika dunia hii iliyosheheni raha na kalaha ,ni mazishi ya mzee Samwel Ntambala Luangisa.Kutokana na wingi watu walifika, wengi wao walijikuta wakishuhudia maziko kwa kuangalia Tv zilizokuwa zimefungwa katika kila kona ya maeneo ya maziko,Sifa rukuki na salamu za rambirambi zilitolewa zikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw John Mongella alieanza kwa salamu za rais Jakaya Kikwete,viongozi mbalimbali wakiwemo wa kidini, ndugu na marafiki kila aliesimama hawakusita kudadavu sifa rukuki za marehemu wakati wa uhai wake,ukiondoa kushika madaraka makubwa akiwa kati ya miaka 29 na 30 tena kipindi cha rais wa awamu ya kwanza Mwl Nyerere marehemu alikuwa na sifa kubwa ya kupenda mdogo na mkubwa, tajiri na masikini lakini kikubwa zaidi alitetea haki za watu,Hakika naweza kesha nikieleza kile kilichojiri lakini kwa ufupi ndugu msomaji tambua kuwa ulikuwa ni msiba uliosheheni majonzi,simanzi kwa wengi.
Wa pili kushoto ni mjane wa marehemu Ma Geretu akitatua mgogolo wa wajukuu wakidai haki yao,hii ni kabla ya mazishi,dola za kutosha zilihusika na wajukuu wakatulia.
Hakika kitu miwani kilihusika kwa wengi.
Balozi Kagasheki akisalimiana na Bw Geroge Kalunde mwenyekiti wa mazishi.
Kitu miwani kilichukua kasi kubwa.
Viongozi wa dini walimzungumza marehemu walivyomfahamu.
Wakati yakitolewa maelezo ya marehemu ulifika wakati watu walilizimika kucheka na kufurahi kwa kumkumbuka.
Watoto wa marehemu.
Hakika wauza miwani hawatomsahau mzee Luangisa.
Bw Novatus Nkwama mwenyikiti ccm Bukoba vijijini.
Baba Askof wa kanisa la Authodox.
Vilio wakati wa kuaga mwili vilitawala.
Kushoto, mzee Mashasi, Baba askofu Kilain na Baba askofu wa Authodox.
Abankango,wana ukoo.
Jamani kitu miwani.
Mjane wa marehemu.
Mzee Byolwango akihakiki na kupokea rambirambi.
Mkuu wa Mkoa Kagera Bw John Mongela akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa akitoa rambirambi na kumuelezea marehemu.
Mama Anna Tibaijuka.
Murungi Badru Kichwabuta akitoa shukrani.
Kimjinimjini tunasema Nyomi la kufa mtu.
Watu busy na Tv wakiangalia kinachoendelea.
Watu wakitafuta matukio.
Bukobawadau nae akiyatafuta matukio.
Shekhe Mustafa akiwa na mzee Galiatano.
Padre Mrosa na shekhe wa Mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta.
Bukobasports nae achezi mbali.
Mzee masabala akaeleza enzi zao na marehemu.
Paschazia Barongo akamuelezea mjomba wake alivyowapenda watoto wa ndugu zake,akayataja majina mbalimbali ya marehemu, ila katika yote umati ukacheka alipotaja jina la MBALI ULILIBATA NDIYO NLILIBATA,hakika marehe alikuwa na uwezo wa kumliki jukwaa alipokuwa akihutubia.
Kcu 1990 Ltd wakitoa rambirambi.
Baba Askofu Kilain akitoa neno,katika mengi aliyoeleza hakusita kutamka kuwa marehemu alitetea haki za wanyonge,na aligusia viwanja vyashule ya wasichana Rugambwa vilivyovamiwa na watu kuwa marehemu alitetea virudishwe.
Baba Askof Buberwa.
Umati ukifuatilia matukio kwenye Tv.
Kampuni ya kuzika kutoka Uganda ikaanza kazi yake.
TUTAKUKUMBUKA DAIMA MZEE SAMWEL NTAMBALA LUANGISA,KWA UPENDO WAKO, UCHESHI, HEKIMA NA BUSARA, PUMZIKA KWA AMANI.