Friday, 1 November 2013

TBL YAFANYA HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA MASHINDANO YA MITUMBWI MKOA WA KAGERA YANAYODHAMINIWA NA BIA YA BALIMI

 meneja masoko kanda ya ziwa Sylvester sizya akieleza bia ya balimi kuwa ndio mdhamini wa mashindano ya mitumbwi na kuwaomba wateja  kunywa kwa wingi bia ya balimi kuunga  mkono mashindano hayo
                                                    wadau
 mwenyekiti wa Tanzania canoe Association  Richard Mgabo akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa ufunguzi
 zilipandishwa bendera za TBL kuashiria ufunguzi wa mashindano ya mitumbwi mkoa wa kagera 2-11-2013
                                                                           cheeeeeeers


                                                                muda wa vitafunwa



                                                                        furaha
                                                                    ilikuwa ni burudani shadida
                                                   super mkude akimtunza mnenguaji
                                     bw george lyakulwa  akifurahia na bw rakson kahabuka
                                         ni burudani katika viwanja vya ghara la Tbl bukoba mjini

JIUNGE SASA THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA


THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANA
FACULTY OF ARTS AND SOCIAL SCIENCES
For those who are interested in pursuing studies in any of our programmes in the Faculty of Arts and Social Sciences. In case you are, please contact
(Revocatus B. Biro   Email: revocatus.biro@out.ac.tz  0762 002 919) or direct to Dean Faculty of Arts Social Science's (Dr. Deus Ngaruko  Email:dfass@out.ac.tz  +255 22 2668835) as soon as possible so that we can allocate you to
a programme of your choice subject to meeting minimum entry requirements
in the programme of your choice

Here below are the all seventeen Masters Degrees and Postgraduate Diplomas to be offered by FASS during the 2013/14 academic year.
  1. Master of Social Work (MSW) –(Hybrid mode)-Executive
  2. Master of Science in Economics- (MSc. Economics)-Evening and Executive
  3. Master in Community Economic Development(MCED) -Evening and Executive
  4. Master in Tourism Management and Planning (MTMP) – Thesis, Evening and Executive
  5. Master of Arts in History (MA. Hist)- Thesis, Evening and Executive
  6. Master of Arts in Natural Resource assessment and Management (MNRAM)- Distance, Evening and Executive
  7. Master of Arts in International Development and Cooperation (MA ICD)-Evening and Executive
  8. Master of Science in Humanitarian Action, Cooperation and Development (MSc HACD)- Evening and Executive
  9. Master of Arts in Governance and Leadership (MA GL)-Evening and Executive
  10. Master of Arts in Kiswahili (MA Kisw)-Thesis, Distance, Evening and Executive
  11. Master of Arts Linguistics (MA Ling)- Thesis
  12. Master of Arts in Geography (MA Geogr)- Thesis
  13. Master of Arts in Economics (MA (Econ) –Thesis
  14. Master Arts in Sociology  (MASO)-
  15. Master of Arts in Project Management
  16. Post Graduate Diploma in Social work (PGDSW)- Hybrid and Distance
  17. Post Graduate Diploma in Policy Studies (PGDPS) Evening and Executive

Thursday, 31 October 2013

*WABUNGE WAKUSANYA SAINI ZA KUTAKA KUMN'GOA SPIKA ANNE MAKINDA



Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka na Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msola katika Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana. 
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
“Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?” chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa,” alisema Dk Kashililah.
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
“Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo,” alisema Dk Kashililah.
Kuhusu Serukamba
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
“Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake,” kilisema chanzo hicho.

ALHAJI TAUFICK SHARIF APOKELEWA LEO UWANJA WA NDEGE BUKOBA

                                                                          Alhaji Taufick sharifu
                        Vip bukoba airport viongozi wa dini wakisubiri kumpokea alhaji taufick sharifu
                                                 Alhaji Taufick sharifu akishuka kwenye ndege
                                mke na mtoto wa alhaji Taufick wakiwa na furaha uwanja wa ndege
                                                            karibu mme wangu, ni furaha
                                                             shekhe kichwabuta akimpokea alhaji Taufick
                                                   umati uliokuwa nje ya uwanja ukimsubiri alhaji
                                                                          picha ya pamoja
                                                  msafara kutoka airport kuelekea nyumbani
                                                                  alhaji akiswali msikiti wa bilele
                                                                                      alhamdulilah
                                                       alhaji chuchu na bw majid kichwabuta
                                                                                    nyumbani
                                                                                dua
                                                    wamama walikuwa kibao
                                                                           alhaji kagire
                                                                 wakati wa kupata riziki ulifika
                                                                 muda wa chakula ukafika