Monday, 28 October 2013

*RAIS KIKWETE AITAKA JAMII KUJENGA TABIA YA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakimpongeza mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi kwa ahadi ya kuichangia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama Jumla ya Shilingi milioni mia mbili kila mwaka kwa miaka mitano,wakati mahafali ya kwanza ya shule hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Nyamisati,wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mishoni mwa Wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA NakayMA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau akimkabidhi tuzo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake wa kuimarisha elimu nchini wakati wa mhafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyofanyika huko.Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mwishoni mwa wiki.Kuliua ni Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete. Picha naFredy Maro
************************************************************
 NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS  Jakaya Kikwete ameitaka   jamii  kuwa na tabia  ya  kuwafadhili  watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira magumu   katika kuwapatia elimu, chakula na malazi ili waweze kuendesha maisha yao kwa kujiajiri au kujariwa kwani kwa kufanya hivyo nguvu kazi  ya taifa  haitaweza kupotea.

Kauli hiyo ilitolewa jana (juzi) na Rais Kikwete  wakati wa mahafali  ya  kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari  ya  Wama Nakayama iliyoko  Nyamisati , wilayani Rufiji , mkoani Pwani yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Shule hiyo  inayoendeshwa  na Taasisi ya Wanawake  na  Maendeleo(WAMA)  ,ambapo Mwenyekiti wa taasisi hiyo ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 

Rais Kikwete aliwashukuru watu mbalimbali walichangia shule hiyo kwa moyo wao wa upendo na huruma  ili watoto wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira magumu  waweze kupata elimu, huku akisema  kama wasi wafadhili  hao isingekuwa rahisi watoto hao kuwezeshwa kusoma shuleni hapo.

“ Mtapata fadhila  kwa Mwenyezi Mungu  kwa kila mtoto atakayesoma hapa…Mkopesheni Mwenyezi Mungu atawapa fadhila zake,”alisema Rais Kikwete.
 Kauli hiyo pia iliungwa na  mkono na Mama Salma Kikwete ambaye alisema bila juhudi za pamoja kati ya  Serikali, jamii na sekta  binafsi  watoto  wengi wa kundi hilo  watakosa elimu.

Mama Kikwete alisema nchi ina Watanzania milioni 44.9 kama wapo wenye uwezo wapatao milioni tano kila mmoja akimchukua mtoto mmoja. 

“ Tanzania   isiyokuwa  na watoto wasio matumaini inawezekana,”alisema Mama Kikwete  huku akisema kwa kufanya hivyo kuwasaidia kujikwamua katika hali ya umasikini.
    
 Rais   Kikwete   aliwataka wanafunzi  hao  kuwa na malengo ya kupata elimu  ya juu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali na kulisaidia taifa, huku akisisitiza  wawe jasiri kusoma fani  ambazo wanawake wengi wanaogopa kuzisoma   ambazo zitawawezesha kuwa mabingwa mafano udaktari, wahandisi na wanasheria.

 “ Hamna budi kushukuru na kujipongeza ombi langu ni kuweni watoto wema heshima na mabalozi wa shule hii.  Shule hii itakapokamilika huduma zitakuwa bora.Shule hii ina kila sababu ya kuwa shule bora,” alisema Rais Kikwete.

Aidha  Rais Kikwete  alizitaka  halmashauri nchini  kuendelea kushishirikiana  na Maendeleo(WAMA) kuwatambua watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira  magumu  ili  waweze kupata elimu kwa malengo ya  taasisi hiyo.

Katika mahafali hayo Mwenyekiti wa  kammpuni  za IPP, Reginald Mengi  aliahidi kuchangia shule hiyo Sh. milioni 200 kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano na Umoja wa Wanawake Tanzania  wa Chama  cha Mapinduzi (UWT)uliahidi kutoa Sh. milioni 10  yakiwemo mashirika mbalimbali yaliyoahidi kutoa michango  kadhaa.

Rais  Kikwete katika mahafali hayo aliwatunuku vyeti wanafunzi 67 na kutoa zawadi za vyeti na fedha tasilimu kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri, ambapo mwanafunzi  aliibuka mshindi baada ya kufanya vema  kwenye masomo ya biashara, historia na Kiingereza.Mwanafunzi aliyefanya vizuri kila somo alipata Sh. 100,000 na mwalimu Sh. 500,000.  

No comments:

Post a Comment