Saturday 1 February 2014

MWENYEKITI WA CCM TAIFA AWASILI MKOANI MBEYA TAYARI KWA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI


 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano akipunga mkono wakati akishuka kutoka kwenye ndege jioni ya leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kwa sherehe za kuzaliwa kwa CCM zitakazofanyika tarehe 2 Februari ambapo asubuhi kutakuwa na matembezi ya mshikamano kisha kuhitimishwa kwenye uwanja wa wa Sokoine.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe tayari kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 37ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndugu Abdallaha Bulembo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kwa sherehe za kutimiza miaka 37 tangia kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Mjini Ndugu Ephraim Mwaitenda kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya.
 Boda Boda zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete aliyewasili mkoani Mbeya kwa ajili ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

 Bodaboda zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete(katikati) akiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa wa Mbeya tayari kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa wa Mbeya.

MANGULA APEWA SOMO NA MUJATA MBEYA


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wake na Wanachama wa Mujata uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya uliopo Sokomatola Jijini hapa.

Viongozi wa Mujata wakiwakilishwa na machifu wa mkoa wa Mbeya wakimvisha Shuka Makamu Mwenyekiti kama ishara ya kumkaribisha Mkoani Mbeya na kuwa Mlezi wa Mjata popote aendapo.



Mwenyekiti wa Mujata, Chifu Shayo Soja Masoko akimkabidhi Zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM

Wajumbe wa Mkutano kati ya Mujata na makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula wakifuatilia kwa makini Risala inayosomwa na Katibu wa Mujata Uswege



ASASI ya Muungano wa Jamii Tanzania(MUJATA) imekishauri Chama cha Mapinduzi (CCM) mambo yanayochangia kudhoofisha Chama na kutoa mwanya kwa vyama vya upinzani kupata nguvu na kukubalika katika jamii tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Ushauri huo ulitolewa na Asasi hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wake na Wanachama wa Mujata uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya uliopo Sokomatola Jijini hapa.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Mujata, Chifu Shayo Soja Masoko, ambaye alimwambia Makamu Mwenyekiti kuwa Chama kikitaka kuendelea kutawala na kukubalika katika jamii jinatakiwa kufanya utafiti kabla ya kuteua wawakilishi wa wananchi katika maeneo mbali mbali.
Alisema Chama kikifanya utafiti wa mtu anayekubalika katika jamii bila kujali uwezo wake wa kifedha na  elimu na kumchagua kuwa mwakilishilishi wao itasaidia kuondoa makundi, Rushwa na vurugu katika jamii kutokana na makao makuu kuteua watu wasiokubalika na jamii.
Aidha katika Risala yao kwa Makamu Mwenyekiti, Mujata walitoa maoni mbali mbali ya namna ya kukijenga chama na kuendelea kuaminiwa na Watanzania ambayo ni pamoja na Chama kuwapa uongozi ndani ya chama baadhi ya watu wanaoshindwa kuhoji utendaji wa Serikali kwa ngazi za uenyekiti na katibu katika ngazi ya Shina.
Pia walishauri chama kudhibiti baadhi ya wagombea wanaotumia fedha ili kupata madaraka hata kama hawakubaliki katika jamii na uongozi kuendelea kuyafumbia macho bila kuwachukulia hatua zozote na kufanya nchi kukithiri kwa rushwa.
Akijibu baadhi ya mambo yaliyoko kwenye Risala hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, Philip Mangula, alisema Chama kina utaratibu wake wa kushughulikia wanachama wanaokiuka kanuni za chama kwa maksudi kwa kuwaita na kuwaonya kwa misingi ya Katiba ya Chama.
Alisema katika Siasa hakukosekani Machangudoa kamawalivyo mitaani ambao kazi yao ni kujipisha pitisha bila kujali utaratibu na kuongeza kuwa jamii inatakiwa kuwadharau kabisa na kwamba hata chama hakikubaliani na hali hiyo.
Mangula alisema Wanasiasa duniani kote ndiyo waanzilishi wa migogoro katika jamii  kutokana na kukosa Sera za kuwaambia  wananchi wake hivyo kulazimisha kuonekana kwa kutumia njia zisizohalali ikiwemo kuwachonganisha wananchi.
Aliongeza kuwa wanaotafuta uongozi kwa kutumia fedha ni halali kwamba hawana uwezo na hawajiamini ndiyo maana huna mbinu mbadala ya kulamisha kukubalika ni kutumia fedha jambo ambalo linazalisha taswira mbaya katika Taifa.
Aidha Mangula ambaye katika Mkutano huo alivisha Shuka kama ishara ya kuwa Mlezi wa Chama cha Jamii popote nchini, alikipongeza chama hicho kwa jinsi walivyofanikiwa kuzima baadhi ya matukio ya uhalifu Mkoani Mbeya na kuondoa dhana mbaya iliyokuwa ikijulikana kuhusu Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya mambo waliofanikiwa kudhibiti na kuyakomesha kabisa ni pamoja na Uchunaji wa Ngozi, Mauaji ya Watoto, Upigaji wa nondo, wananchi kujichukulia Sheria mikononi, Maandamano yasiyokuwa na tija katika jamii, Vurugu zinazochochewa na vyama vya Siasa na viongozi wa dini likiowemo suala la Uchinjaji wa Nyama.

Friday 31 January 2014

MAMIA WAMZIKA MAREHEMU ABDALLAH NZOMKUNDA 31-1-2014

 Waumini wa kislamu na wananchi wakielekea makaburi ya kishenge
 Mazishi yakiendelea
 Umati mkubwa wa watu waliojitokeza kumzika
 Baada ya mazishi  walihitimisha nyumbani na mambo yakawa hivi
 Mambo ya pilau

OMG..WAVAA VIMINI NA NGUO ZA NUSU UTUPU JIJI LA ARUSHA KUKIONA CHA MTEMA KUNI0...!NI BAKORA TU....!

MKUTANO Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru umeazimia kuwachapa viboko vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake.
wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.

Mkutano huo umepitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima kijijini Olgilai limefikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa nguo zisizo na heshima. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24 mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao. 

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza: 

“Viongozi wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote wakubwa kwa wadogo.” 

Katika barua yake ambayo MTANZANIA inayo nakala yake Mwenyekiti huyo alisema kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hili na kuamuru lianze kutumiwa Januari 24 mwaka huu. 

Aliyataja maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko. 

Jingine ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama. 

“Vijana wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa viroba, uchezaji kamari na karata. 

“Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani watashughulikiwa,” alisema Boazi.

KAMA HUKUWAHI KUIONA VIZURI NDEGE YA RAIS WA TANZANIA, TAZAMA PICHA ZAKE HAPA



Hii ndio Ndege ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambulika kama 5H - ONE

Thursday 30 January 2014

BREAKING NEWS... BIBI KIZEE ANAESADIKIWA NI MCHAWI AKUTWA CHUMBANI KWA MTU, MAENEO YA HAMUGEMBE BUKOBA

 Ni bibi kizee ambae hatukupata jina lake anaetuhumiwa kuwa mchawi
 Polisi wakitoa msaada wa kumnusuru bibi kizee aliekutwa chumbani kwa mtu
 Bibi kizee akipandishwa kwenye gari la poilisi
 Majanga kweli kweli
 Gari la polisi likiondoka eneo la tukio
 Akishushwa kituo cha polisi Bukoba
AKIINGIA KITUO CHA POLISI
 Bibi kizee akiingizwa mahabusu
Bw Bosco  ambae ni jirani wa eneo lilitokea tukio, ambae ameeleza kuwa alijitahidi sana kuwasihi wananchi wasimpige huyo bibi anaetuhumiwa kuwa mchawi na kutoa taarifa kituo cha polisi