Friday 26 June 2015

SAFARI YA MWISHO YA MA KALOLINA LAULIAN MWILILIZA,AACHA WAJUKUU 51 NA VITUKUU 44

 Ni ibada ya misa ya mazishi ya marehemu Ma Kalolina Laulian Mwililiza aliezikwa katika kijiji cha Ruhunga Bukoba vijijini,Marehemu aliezaliwa mnamo 5-8-1923 na kufariki 21-6-2015,amefariki akiwa na umri wa miaka 92
 Picha ya marehemu Ma Kalolina Laulian katika uhai wake

 Mzee John akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia.
 Bw Bushira Mc wa shughuli ya maz
Mtoto wa marehemu Bw  Angero Rubalemwa Lauliani.

Thursday 25 June 2015

MSHTUKO!!!Mwakyembe Nitapambana Kufa na Kupona LOWASSA asiingie Ikulu

Waziri wa jumuiya ya ushirikiano wa Afrika Mashariki. Harrison Mwakyembe


WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, ameapa kupambana kufa au kupona, kumzuia Edward Lowassa, kuingia Ikulu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).




Katika andishi lake alilolituma kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Mwakyembe anasema, Lowassa hana sifa ya kuwa Rais wa Jamhuri. Amesema, “…namuona Lowassa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.”
lisema hili bila kukemea jicho wala kuwa na wasiwasi wowote na maisha yangu kwani najiamini na mwenyezi mungu ananilinda na watanzania wananiombea daima na najisikia furaha kuwa miongoni mwa wabunge wa CCM ambao hatukuufumbia macho ufisadi wa kampuni feki la kuzalisha umeme iliyomuhusisha waziri mkuu ambaye mimi namuita aliyejiuzulu na sio kustaafu.
Nakushauri ujitafakari vizuri kwani CCM haitoweza kumkabidhi nduli nchi hii.
Unahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafijiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi?
Hivi hujui watanzania wakushangaa unasema safari ya matumaini wakati safari hiyo ni ndani ya bahari iliyojaa majoka na mizimu ambayo imejivika ngozi ya kondoo ili iwameze katikati ya bahari?
Nitakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.
Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jihanam kuwa peponi, kwa manufaa ya watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya nbwembwe za fedha. Eh mwenyezi mungu nipe uthabiti kwa hilo.

Rai yangu kwa wana CCM na watanzania tuchague viongozi bora na sio kwa nguvu ya fedha, wapambe na kutembelea nyota ya mtu.
Utauficha wapi uso wako wakati ambapo CCM itakapokuangusha kwa kishindo na kuchagua wawakilishi walio safi? Utapata kiharusi na shock bure kwa kupoteza fedha za madili uliyopiga RICHMOND na ufisadi mwingine.

Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb) Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

JANUARY MAKAMBA APATA WADHAMINI 8024 KAGERA,APOKELEWA KWA SHANGWE BUKOBA MJINI NA KUELEKEA UJOMBANI MISSENYE.

 Naibu waziri wa  mawasiliano, sayansi na Teknologia January Makamba akiwa ameambatana na mkewe amewasili katika Mkoa wa Kagera na kupokelewa na mamia ya wananchi katika manispaa ya Bukoba na badae kuelekea wilaya ya Missenye ambako shughuli ya kudhaminiwa ilifanyika.Akiongea kwa nyakati tofauti katika Manispaa ya Bukoba na wilayani Missenye January Makamba amesema ametafakari sana kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais,amesema rais anaetakiwa kwa sasa kwa watanzania ni rais ambae anafikira mpya, mtazamo mpya na ambae anajua matatizo ya wananchi na anaetambua kuwa sasa inatakiwa Tanzania mpya.Mh January amepata wadhamini 8024 katika wilaya ya Missenye.
 Akiwasili uwanja wa ndege Bukoba.
 Akiwa na mkewe.
 Msafara ukiongozwa na pikipiki kuelekea ofisi za chama Bukoba mjini.
 Umati mkubwa Bukoba mjini
 Mwenyekiti wa uvccm Mkoa Kagera Yahaya Kateme akiwa na January Makamba.
 Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera akimkaribisha.
 Mkewe akisalimia wananchi.
 Missenye.
 Mto Kagera.
 Akiwasili Missenye.


























 Mama mzazi wa January Makamba mwenye miwani akimkaribisha mwanae ujombani baada ya kudhaminiwa katika wilaya ya Missenye.