Saturday, 28 June 2014

KAGASHEKI CUP 2014: BILELE 1 vs RWAMISHENYE 3, BINGWA MTETEZI AANZA VIBAYA!! ACHAPWA NA WANA BODABODA RWAMISHENYE FC!

Na Faustine Ruta, Bukoba
Mabingwa watetezi Bilele FC wameanza kwa kufungua Michuano hii ya Kagasheki Cup vibaya baada ya Kutandikwa bao 3-1 na Timu ya Rwamishenye Fc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini. Bilele FC ndio walioanza kuifunga timu ya Rwamishenye katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza, Bao likifungwa na Miraji Ramadhan. 
Timu ya Rwamishenye waliongeza bidii ili wasawazishe bao na katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza walisawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Khalid Seleman na kuongeza tena bao jingine katika dakika ya 42 kupitia kwa Yahaya Sadiq aliyekuwa amevaa jezi namba 7 mgongoni na kufanya 2-1 dhidi ya timu ya Bilele Fc yenye makazi yake Bukoba Mjini wakifaamika zaidi kwa jina la KM.0, hadi mapumziko Rwamishenye ndio walikuwa mbele ya bao 2-1. Kipindi cha Pili dakika ya 56 walioshona tena bao jingine la mwisho kupitia kwa mchezaji wake matata Edwin Edo na kufanya kipute kumalizika kwa bao 3-1. 
Kesho Mtanange unaendelea na utazikutanisha timu za Bakoba na Kashai, Mtanange utakao pigwa saa 10:00 jioni. Jumatatu kutakuwepo na mitanange 2 wa saa 8 na saa 10 jioni.Wachezaji wa Rwamishenye Fc wakishangilia moja ya bao laoWachezaji wa timu ya Bilele Fc wakishangilia bao lao la dakika ya 5 lilifungwa na Miraji RamadhanKikosi Cha Timu ya Rwamishenye kilichoanzaKikosi cha Timu ya Bilele FCTimu zikisalimianaWaamuzi na Timu Kapteni timu zote mbili wakilianzisha Waamuzi wa Mtanange huuKikosi cha Timu ya Rwamishenye uwanjani wakiomba kabla ya kipute kuanza muda mfupiMgeni Rasmi akisalimia timu ya RwamishenyeMgeni Rasmi akisalimia timu ya Bilele Fc ambao ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hiliMgeni Rasmi akiteta jambo na Wachezaji Pande zote mbiliMgeni Rasmi wa pili (kusho) akiteta jambo kwenye ufunguzi  wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued, (kulia) ni Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii jioni.
Mbwembe nazo hazikosi kwenye hii Ligi......
Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi huu wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued alianzia hapa kwa kufungua hii Ligi kwa kumfunga kipa moja wapo kati ya timu hizi mbili.Mashabiki wakishangilia timu yaokipute kikiendelea..kaitabaWachezaji wa Timu ya Bilele walivalia jezi zinazofanana na  Mbeya CityPatashika za hapa na pale zikiendelea, kila mchezaji akitaka aupate mpiraKila Mchezaji alikuwa na mwenzake wakubanana nae.Hapa ukatizi ndugu yangu!Mpira ukiendelea..Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakicheza muziki baada ya kusawazishaMgeni Rasmi kwenye ufunguzi huu wa Mashindano ya Kombe la KAGASHEKI CUP 2014, Mzee Abdul Sued, (kushoto) ni Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii wakifuatilia kwa Karibu.Mashabiki ndio usiseme...walijaa uwanjani KaitabaMashabikiWaamuzi wakina Dada nao walikuwepo wakitazama wenzao wakiendesha mpiraMchezaji wa Rwamishenye akishangilia bao lake la pili lililofungwa na Yahaya
Wachezaji wa Rwamishenye wakishangilia bao lao baada ya kuwanyuka Bilele Fc
Bango la Timu ya Bilele Fc likiwa mbele ya Mashaki wake! wakisema si..si..simnaona!!!!!

Mashabiki baada ya kukutana na Camera..wakajimwaga kivyao!!! Ligi ya Nyumbani!!

Tuesday, 24 June 2014

REDD'S MISS KAGERA 2014 KUPATIKANA 2-8-2014 KATIKA UKUMBI WA LINA'S

 Mratibu wa shindano la urembo Mkoa wa Kagera Jamal Kalumuna amesema maandalizi ya kumpata mrembo Redd's miss Kagera 2014 yanaendelea vizuri na tarehe 2-8-2014 shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Lina's kuanzia saa 2.00 usiku. Mratibu huyo Jamal Kalumuna akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni Lweru Intertaiment  Kaptein Mwasa amesema maandalizi  yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wakazi wa Mkoa wa Kagera wakae mkao wa kula kwa ajili ya kushuhudia mpambano mkali utakao shirikisha warembo 14 kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Kagera. kwa upande wa burudani amesema wanategemea kuwa na wanamuziki wakubwa kutoka nchini Uganda,Kenya na Tanzania na watatangazwa hivi karibuni baada ya kusaini mikataba.Mara baada ya mcuano huu watapatikana washindi watatu wa nafasi za juu wataoshiriki mashindano ya kanda ya ziwa yatakayofanyika jijini Mwanza katikati ya mwezi Agust.
 Mmoja ya warembo waliowahi kutwaa taji la urembo
 Kulia ni Kaptain Mwasa,  Hashimu Rundenga na Jamal kalumuna(jamco) katika moja ya mashindano ya urembo.
 Kamati ya Miss Tanzania wakiwa na waandaji wa Miss Kagera,ni moja ya mashindano yaliyofanyika kipindi cha nyuma.
Hapana kukosa 2-8-2014 KATIKA UKUMBI WA LINA'S

RAIS KIKWETE AMWAPISHA BALOZI NA WAJUMBE WA OPERESHENI TOKOMEZA IKULU DAR




      Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo,kupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

      Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.

      Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi, Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.



       Wajumbe wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal (Wanne Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema (kulia),Wasita kushoto ni  Balozi Joseph Edward Sokoine.





      Picha ya pamoja na Balozi na Wajumbe wa Operesheni tokomeza. Picha na Freddy Maro

      RATIBA YA LIGI YA KAGASHEKI CUP 2014


      KUNDI A
      1. Nyanga
      2. Bakoba
      3. Kahororo
      4. Ijuganyondo
      5. Kashai
      6. Kitendaguro
      7. Hamugembe


      NA.
      TAREHE
      KUNDI
      TIMU ZINAZOCHEZA
      MUDA
      UWANJA
      1.         
      29/06/2014
      A
      Kashai
      Vs
      Bakoba
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      2.         
      01/07/2014
      A
      Nyanga
      Ijuganyondo
      Vs
      Vs
      Kitendaguro
      Kahororo
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      3.         
      03/07/2014
      A
      Hamugembe
      Kahororo
      Vs
      Vs
      Bakoba
      Kashai
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      4.         
      05/07/2014
      A
      Ijuganyondo
      Kitendaguro
      Vs
      Vs
      Nyanga
      Hamugembe
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      5.         
      07/07/2014
      A
      Bakoba
      Nyanga
      Vs
      Vs
      Kahororo
      Hamugembe
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      6.         
      09/07/2014
      A
      Hamugembe
      Kashai
      Vs
      Vs
      Kahororo
      Kitendaguro
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      7.         
      11/07/2014
      A
      Kitendaguro
      Nyanga
      Vs
      Vs
      Ijuganyondo
      Bakoba
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      8.         
      13/07/2014
      A
      Hamugembe
      Kitendaguro
      Vs
      Vs
      Kashai
      Bakoba
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      9.         
      15/07/2014
      A
      Nyanga
      Kashai
      Vs
      Vs
      Kahororo
      Ijuganyondo
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      10.      
      17/07/2014
      A
      Ijuganyondo
      Nyanga
      Vs
      Vs
      Bakoba
      Kashai
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      11.      
      19/07/2014
      A
      Kahororo
      Hamugembe
      Vs
      Vs
      Kitendaguro
      Ijuganyondo
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      Kila kundi zinatoka timu nne kwenda hatua ya Robo fainali.


      MSHINDI KUNDI B NO. 1
      Vs
      MSHINDI KUNDI A NO. 2
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI B NO. 4
      Vs
      MSHINDI KUNDI A NO. 3
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI A NO. 1
      Vs
      MSHINDI KUNDI B NO. 3
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI A NO. 4
      Vs
      MSHINDI KUNDI B NO. 2
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      Tarehe zake zitatangazwa baadae kuwahi muda Uwanjani Kaitaba ni jambo la muhimu sana.




      KUNDI B
      1. Kibeta
      2. Kagondo
      3. Bilele
      4. Nshambya
      5. Rwamishenye
      6. Miembeni
      7. Buhembe
       

      NA.
      TAREHE
      KUNDI
      TIMU ZINAZOCHEZA
      MUDA
      UWANJA
      1.         
      28/06/2014
      B
      Bilele
      Vs
      Rwamishenye
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      2.         
      30/06/2014
      B
      Nshambya
      Kagondo
      Vs
      Vs
      Kibeta
      Buhembe
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      3.         
      02/07/2014
      B
      Miembeni
      Rwamishenye
      Vs
      Vs
      Bilele
      Nshambya
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      4.         
      04/07/2014
      B
      Kibeta
      Buhembe
      Vs
      Vs
      Kagondo
      Miembeni
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      5.         
      06/07/2014
      B
      Miembeni
      Bilele
      Vs
      Vs
      Nshambya
      Kibeta
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      6.         
      08/07/2014
      B
      Kagondo
      Nshambya
      Vs
      Vs
      Rwamishenye
      Buhembe
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      7.         
      10/07/2014
      B
      Kibeta
      Rwamishenye
      Vs
      Vs
      Buhembe
      Miembeni
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      8.         
      12/07/2014
      B
      Bilele
      Miembeni
      Vs
      Vs
      Nshambya
      Kagondo
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      9.         
      14/07/2014
      B
      Kagondo
      Bilele
      Vs
      Vs
      Nshambya
      Buhembe
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      10.      
      16/07/2014
      B
      Buhembe
      Miembeni
      Vs
      Vs
      Rwamishenye
      Kibeta
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba
      11.      
      18/07/2014
      B
      Bilele
      Rwamishenye
      Vs
      Vs
      Kagondo
      Kibeta
      08.00 Mchana 10.00 Jioni
      Kaitaba
      Kaitaba









      Kila kundi zinatoka timu nne kwenda hatua ya Robo fainali.

      MSHINDI KUNDI B NO. 1
      Vs
      MSHINDI KUNDI A NO. 2
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI B NO. 4
      Vs
      MSHINDI KUNDI A NO. 3
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI A NO. 1
      Vs
      MSHINDI KUNDI B NO. 3
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      MSHINDI KUNDI A NO. 4
      Vs
      MSHINDI KUNDI B NO. 2
      10.00 Jioni
      Kaitaba
      Tarehe zake zitatangazwa baadae kuwahi muda Uwanjani Kaitaba ni jambo la muhimu sana.