Tuesday 24 June 2014

REDD'S MISS KAGERA 2014 KUPATIKANA 2-8-2014 KATIKA UKUMBI WA LINA'S

 Mratibu wa shindano la urembo Mkoa wa Kagera Jamal Kalumuna amesema maandalizi ya kumpata mrembo Redd's miss Kagera 2014 yanaendelea vizuri na tarehe 2-8-2014 shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Lina's kuanzia saa 2.00 usiku. Mratibu huyo Jamal Kalumuna akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni Lweru Intertaiment  Kaptein Mwasa amesema maandalizi  yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wakazi wa Mkoa wa Kagera wakae mkao wa kula kwa ajili ya kushuhudia mpambano mkali utakao shirikisha warembo 14 kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Kagera. kwa upande wa burudani amesema wanategemea kuwa na wanamuziki wakubwa kutoka nchini Uganda,Kenya na Tanzania na watatangazwa hivi karibuni baada ya kusaini mikataba.Mara baada ya mcuano huu watapatikana washindi watatu wa nafasi za juu wataoshiriki mashindano ya kanda ya ziwa yatakayofanyika jijini Mwanza katikati ya mwezi Agust.
 Mmoja ya warembo waliowahi kutwaa taji la urembo
 Kulia ni Kaptain Mwasa,  Hashimu Rundenga na Jamal kalumuna(jamco) katika moja ya mashindano ya urembo.
 Kamati ya Miss Tanzania wakiwa na waandaji wa Miss Kagera,ni moja ya mashindano yaliyofanyika kipindi cha nyuma.
Hapana kukosa 2-8-2014 KATIKA UKUMBI WA LINA'S

No comments:

Post a Comment