Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya mradi wa maji wa Kwamtokama ulioko Kata ya Chikonji Wilayani Lindi
kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Don Consult Limited Ndugu
Ahmed Salum (kulia) huku baadhi ya wananchi wakichota maji kuhusu
utekelezaji wa mradi. Mradi huo utakapokamilika utanufaisha wananchi
waishio katika vijiji vinne vilivyopo katika kata hiyo ambavyo ni
Chikonji Kaskazini na Kusini, Jangwani na Nanyanje vyenye wakazi wapatao
7000.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa kutoka Lindi Mjini Mama Salma Kikwete
akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Chikonji Kusini
waliofika kuchota maji baada ya Mama Salma kutembelea chanzo hicho juzi.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
**************************************************
*MAMA SALMA AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUKWEKEZA KATIKA ELIMU
YA WATOTO
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wazazi
na walezi wilayani Lindi mjini wametakiwa kuwekeza katika elimu
ya watoto wao kwa kuhakikisha wanakwenda shule kwa wakati kwani elimu
ni ukombozi wa maisha na kuolewa katika umri mdogo kwa watoto hao
hakutawasaidia kimaisha.
Mwito
huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati
akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya
Chama hicho katika matawi yaliyopo kweye kata za Chikonji,
Tandangongoro na Ng’apa wilaya ya Lindi mjini.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ni
jukumu la mzazi na mlezi kusimamia elimu ya mtoto wake pamoja na kumpa
malezi mazuri kwa kufuata malezi ya zamani yanayoendana na mila na
utamaduni wa mtanzania kwani hivi sasa kutokana na utandawazi mienendo
ya vijana wengi siyo mizuri.
MNEC
huyo pia aliwataka watoto waliofika kumsalimia mara baada ya kumaliza
mkutano wake wa ndani na viongozi hao wa CCM kusoma kwa bidii na kuacha
tabia ya utoro kwani elimu pekee ndiyo itakayowakwamua na hali ngumu ya
maisha.
Aidha
Mama Kikwete aliwahamasisha viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM
kujiunga katika vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuandika maandiko
ya kibiashara ili wapate mkopo kutoka Serikalini na kuweza kufanya
miradi kama ufugaji wa kuku, mamalishe, ufundi seremala, kwa
kujishughulisha na biashara hizo watakuwa wamejikwamua kiuchumi.
“Mkijiunga
katika vikundi vya ujasiriamali mtaweza kukopa fedha kutoka Serikalini
jambo la muhimu mkumbuke kuwa fedha hizi hampewi bure mnatakiwa
kuzirudisha ili na wenzenu waweze kukopa”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wa Afya aliwahimiza kina mama kujitokeza kwa wingi kupima afya
zao ikiwemo saratani ya matiti na shingo ya kizazi ambayo inatibika
ikiwa itagundulika mapema mgonjwa atapata matibabu na kupona.
“Hivi
sasa kuna maradhi mengi ikiwemo saratani ya matiti na shingo ya kizazi
msiogope kwenda kupima na kujua afya zenu. Nanyi kinababa wahimize
wake zenu wakapime ugonjwa huu, mkiona dalili wawapeleke Hospitali
mapema kwani ugonjwa huu unatibika kama mgonjwa atawahi mapema kupata
matibabu”, alisisitiza.
Alimalizia
kwa kuwataka viongozi hao kuonyesha mfano kwa wananchi kwa kujenga
nyumba bora za matofali ya kuchoma na kuezeka kwa bati na siyo za miti
kwani moja ya sera ya CCM ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira
na kutokukata miti hovyo.
Akiwa
katika Kata ya Chikonji MNEC huyo alikagua mradi wa maji wa Kwamtokama
na kujionea maendeleo ya mradi huo ambao ukikamilika utawanufaisha
wananchi wapatao elfu saba kutoka vijiji vya Jangwani, Nanyanje ,
Chikonji Kusini na Kaskazini.
Mama
Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini
alikutana na viongozi hao wa Halmashauri kuu ya matawi ya CCM katika
matawi ya Chikonji Kusini na Kaskazini,Nandambi, Kilolombwani na
Cheleweni kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na
kufanya vikao vya ndani na viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya mwaka 2010
No comments:
Post a Comment