Hili ndio kanisa la kilutheri usharika wa Kashura Bukoba Manispaa lenye zaidi ya miaka mia moja tangu lijengwe na sasa litaanza kufanyiwa ukarabati hivi karibuni.
Mzee Reginald Mengi,kupitia kwa Mbunge wa jimbo la Bukoba Balozi Khamis Kagasheki ametoa ahadi ya kiasi cha shilingi milioni kumi kusaidia ukarabati wa kanisa.
Mh Balozi Khamis Kagasheki ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye Ibada maalumu na harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Kashura.akielezea kupokea mwaliko huu alibahatika kukutana na Mzee Reginald Mengi akiwa Dar-es-salamu na alimjulisha mwaliko wake wa kuwa mgeni Rasmi katika harambee yauchangiaji ukarabati wa kanisa alimwambia kupitia kwake atachangia kiasi cha shilingi milioni kumi.
Mchungaji wa kanisa la usharikika wa kashura Alex Kasisi katika maubiri yake amewasihi waumini na watu wote kwa ujumla kuwa makini sana na Ulimi na hasa unapokuwa unazungumza.Ulimi umekuwa ukichonganisha watu, ulimi umekuwa ukivunja ndoa za watu, ulimi umikuwa ukisababisha uvunjaji wa amani katika maeneo mengi.
Wanafunzi wa Josiah Girls high school wakiwa kwenye shughuli, uongozi na shule umechangia kiasi cha laki moja.
Washarika
Mtangazaji wa Kasibante Redio Nicoras Ngaiza akirusha moja kwa moja LIVE Matangazo kutoka kanisani
Ndugu Ruge Masabara (katibu wa kamati ya maandalizi) akiwa na mkewe
Mzee byolwango mwanakwaya mahiri wa kwaya ya vijana usharika wa kashura
Kushoto ni Katibu mkuu wa ELCT NWD Mchungaji Elmeck Kigembe akiwa na Mchungaji wa kanisa la Kashura Alex Kasisi
Katikati ni Askofu mstaafu Mushemba
Kushoto ni Naibu katibu mkuu ELCT NWD Jonas Rwezaura.
Wazee wakimpongeza mgeni rasmi baada ya kutangaza ahadi ya milioni kumi za Mzee Reginald Mengi
Mnada wa vitu mbalimbali
Tv nchi 32 iliyotolewa na Mzee Jonas Masabara yenye thamani ya 1,065,000 ilinunuliwa na mgeni rasmi kwa kiasi cha 2,800,000 na tv hiyo mh Balozi kagasheki mgeni rasmi alimpa zawadi Katibu mkuu wa ELCT NWD Mchungaji Elimeck Kigembe kwa matumizi yake ya nyumbani.
Waumini wakishangiria baada ya mgeni rasmi kuinunua tv
Mgeni rasmi akimkabidhi tv Katibu mkuu wa ELCT
Mgeni akikabidhi pesa kwa bw Musheshe
Bw Stanley Byolwango akikusanya taslimu
Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Seif Mkude akichangia harambee kumuunga mkono mgeni rasmi ambae ni mlezi wa wanaveterani Bukoba
Bingwa akimpongeza Balozi Kagasheki
Mgeni rasmi Balozi Khamis Kagasheki akiagana na Uongozi wa Kamati ya maandalizi .
Ruga Masabala... miss u my brother
ReplyDelete