Ofisi
ya mkuu wa jeshi la polisi (OCD) pamoja na nyumba za makazi ya askari
polisi vimebomolewa na kampuni inayojenga barabara hiyo China Henan
International Group (CHICO) ndiyo iliyoendesha zoezi hilo la bomoabomoa
chini ya usimamizi wa F.F.U baada ya maaskari polisi kudaiwa kugoma
kuhama.
Katika
hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa
kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha
wilaya pamoja na nyumba wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe
mkoani Kagera kupisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka
Kyaka wilayani Missenyi hadi Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha
lami.
Ni
tukio lililovuta umakini wa watu wengi huku minong'ono ikitawala ya
ukosoaji wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji
maana yake kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U
kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.
Meneja
wa TANROADS mkoa wa Kagera John Kalupare alipopigiwa simu kuelezea
tukio hilo amesema yupo safarini Dar es Salaam na asingeweza kuzungumzia
suala hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa simu
juu ya tatizo hilo, simu yake imeita bila kupokelewa.
Mmoja
wa maofisa wa TANROADS aliyekuwa anasimamia zoezi hilo ambaye hakupenda
jina lake litajwe, amesema kuwa wao wanaonesha mipaka ya barabara na
polisi wanabomoa nyumba zao.
Sisi
TANROADS tunaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao na
kituo chao hivyo waulize wao kwanini ubomoaji unafanywa chini ya ulinzi
mkali amesema.
Hata
hivyo zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na
kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku
dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa
na nyuki hao.
Ni
tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye
dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa
sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U
kulisimamia.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo
ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo baadhi
ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya
Karagwe na Kyerwa.
Chanzo: Malunde1 Blog
No comments:
Post a Comment