Sunday, 31 August 2014

UMEWAHI KUTEMBELEA MAPOROMOKO YA KYAMUNENE? VICTOR ALCARD BWANA HARUSI MTARAJIWA AFANYA UTALII WA NDANI NA RAFIKI ZAKE BUKOBA.

 Kampuni ya Utalii Mkoa wa Kagera Kiroyera Tours imekuwa ikiweka jitihada kubwa sana  kutangaza vivutio vilivyomo katika Mkoa wa Kagera na kuelimisha jamii kwa ujumla kutambua na kuelewa kuwa Utalii unaweza kuufanya  wewe binafsi au Familia si Wazungu tu.Meneja wa Kiroyera Tours Ndugu Willam Ruta(Willy Kiroyera) amekuwa akihimiza  jamii kila mara kufanya utalii wa ndani si kusubiri wazungu tu. Haya yamedhihirishwa na Bw Victor Alcard mkazi wa Bukoba anaeishi Jijini Dar ambae amekuja kwa ajiri ya Send off  ya mchumba wake wanaotarajia kufunga pingu za maisha 13-9-2014 Jijini Dar, yeye na rafiki zake wamefanya utalii wa ndani kutembelea maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba.
 Bw Victor akiwa na swaiba wake wakifurahia hewa safi  na kelele za maji katika maporomoko ya kyamunene maeneo ya kata ya Ijuganyondo barabara ya Maruku kwenye msitu wa Kyamunene Bukoba.
 Bw Victor  akiwa na Jamco mmiliki wa  Kampuni ya Jamcovideo production,Jamcobarbershop na blog ya Jamco.
 Hakika Victor alijipanga ameambatana na wapiga picha maarufu kutoka Jijini Dar kampuni ya Pixelbase na mwwenye miwani ndio mkurugenzi Bw  Abdul Mohamed.wakipeana mikakati ya Send off ya mchumba wa Victor.
 Bw Victor na wanae wakiingia Jamcobarber shop kwa ajili ya usafi
 Huduma zikiendelea
 Kijana wa Pixelbase akiendelea na kazi ya kuchukua matukio.
 Kijana Kevin kutoka JAMCO VIDEO PRODUCTION(kushoto) akiwa na mtaalamu Zungu kutoka Pixelbase ya Dar wakishare love
 Bw Harusi mtarajiwa akipendezeshwa
 Ni Mapozzzzzz
 Ni Mikakati tuuuu
 Mdau ndani ya msitu wa kyamunene
 Victor akiwa katika Msitu wa Kyamunene akifanya utalii wa ndani
 Watu wakifanya utalii
 Ni eneo muhimu sana ukiwa Bukoba akikisha unafika usisimuliwe
 Hali ya hewa safi, upepo mzuri utapenda mwenyewe
 Ukafika wakati raha zikazidi na watu wakatunga wimbo na kuimba kyamunene ni balaaaa
 Bonge la Tour si mchezooo
 UNAONA HIYOOOOO
 Wapiga picha crips zikatosha wakataka  wapigwe picha na wao
 Hapana chezeaa Bukoba wewe...
 Bukoba is beautful,tujivunie
 Wadau kutoka DAR na wengine wa Bukoba  wakifurahia Bukoba.
 Mandhari ya Mji
 Mshikaji Bukoba ni bonge la vitu hadimu duniani....
Hakika Bukoba ni pazuri,hebu anza wewe kutambua uzuri wa Bukoba na kuitangaza,sie jamcobukoba.blogspot.com tulisjaanza,na tutaendelea kuitangaza Bukoba.Hongera Victor kuwa mmoja wa wadau kutembelea vivutio vilivyopo Bukoba.

No comments:

Post a Comment