Friday, 2 August 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KIONGOZI WA TAASISI YA IYF YA KOREA KUSINI NA UJUMBE WAKE

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na ujumbe wa IYF Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadili chapisho la kitabu na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni mkaliman
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Ock Soo Park Ikulu jijini Dar es salaam

BAADA YA ROSE NDAUKA KUHUSISHWA KATIKA FUMANIZI...!! HAYA NDIYO MANENO YA MCHUMBA WAKE ROSE KUHUSU SAKATA HILO

Friday, August 2, 2013



BAADA ya msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kuripotiwa kufumaniwa akiingia gesti na msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub 'Dogo Nasry' huku akiwa amevaa baibui kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, mumewake mtaarajiwa Maliki Bandawe 'Chiwaman' amjia juu msanii huyo kwa madai ya kumchafua mpenzi wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Chiwaman aliweka wazi kuwa msanii huyo Nasry ambaye alimuomba Rose aweze kushiriki kwenye video yake, walishindwa kufikia maamuzi kutokana na kiwango cha malipo kuwa madogo, na badala yake msanii huyo alimuomba wapige picha kama ukumbusho.

Alisema kuwa kitendo hicho cha kupiga picha na msanii huyo wakati wapo katika mazungumzo ya awali ya kukubaliana malipo ndizo picha alizotumia msanii huyo na kudai kuwa alikuwa naye nyumba ya wageni kitendo ambacho si cha kweli.

"Hawa wasanii wachanga wanatafuta umaarufu vibaya kwa kuwachafua watu, ilikuwa amemuomba Rose ashiriki kwenye video yake na ndipo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo hayo na alikuwa na mdogo wangu sasa hapo masuala ya gesti yametokea wapi" alisema Maliki.

Aliongezea kuwa "kama nilikuwa sijui hicho kitu na kwa jinsi mambo yalivyokuwa ningeweza kumuacha mchumba wangu ninayempenda kwa dhati, ila msanii huyo alichokifanya siyo jambo sahihi, kwani alimuomba apige naye picha na Rose alikubali huku bila kujua nia yake ".

Maliki alisema kuwa huyo msanii anatafuta umaarufu kwa kuchafua majina ya watu wengine, kitu ambacho hakina mashiko kwenye jamii.

Thursday, 1 August 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AONDOKA BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI



 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Meya wa Jiji la Dar es salaam Mstahiki Dkt Didas Masaburi wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Mwenyekiti wa CCM wa Dar es salaam Ndugu Madabida Masaburi wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini  Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na waziri wa maliasili na utalii balozi khamis kagasheki  wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick  wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.
Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni wake huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.
 Wasanii wakishangilia wakati ndege iliyomchukua Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra ikipaa wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini Agosti 1, 2013.

MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU JIJINI NAIROBI

Thursday, August 1, 2013

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake kutoka nchi za Maziwa Makuu, wakati walipokuwa katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu, alipoiwakilisha Tanzania katika majadiliano ya mkutano huo uliofanyika Jijini Nairobi, 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Asha Bilal, (wa pili kulia) Balozi wa Tanzania Nchini Kenya, Dk. Batrida Burian, na viongozi wengine wakati alipowasili Jijini Nairobi juzi Julai 30, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu, uliofanyika Jiji humo jana Julai, 31, 2013. Makamu anaondoka leo Jijini Nairobi kurejea nchini baada ya kumalizika kwa majadiliano hayo. Picha na OMR  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika jijini Nairobi Kenya, jana Jumatano ya tarehe 31, 2013. Mkutano huu ulihudhuriwa na Mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Mwenyekiti wa nchi za Maziwa Makuu na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Katibu Mtendaji wa Kamisheni yas Nchi za Maziwa Makuu Prof.Ntumba Luaba, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, wawakilishi wan chi za DRC, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
 
Mkutano huo umepokea taarifa kutoka kwa Mawaziri wa Ulinzi kutoka katika nchi za Maziwa Makuu ambayo imepokelewa na kisha kujadiliwa. Pia ripoti kutoka kwa Kamati ya Kimataifa inayoshughulikia suala la Mazungumzo kati ya Serikali ya Kongo (DRC) na wapiganaji wa kikundi cha M23 kinachojihusisha na upingaji wa serikali ya DRC kikifanya machafuko katika Mashariki mwa Kongo (DRC) imepokelewa kujadiliwa na kisha kupitishwa mapendekezo ambayo nchi washiriki zimeyasaini.
 
Wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, nchi washirika walisisitiza kutaka kuona amani inapatikana katika nchi za Maziwa Makuu na hasa DRC, Afrika ya Kati na Sudan. Wawakilishi hao walielezea kusikitika kwao kutokana na machafuko ya amani katika nchi hizo na wakawataka viongozi mbalimbali wanaotajwa kuhusika na machafuko haya kutambua kuwa athari inayotokana na machafuko haya ni kubwa na inaathiri wananchi wengi.
 
Viongozi hao walisema, nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinahitaji utulivu na kwamba mgogoro wa uvunjaji amani katika Kongo DRC unaotokana na kuwepo kwa kikundi cha M23, lazima upewe tiba ya kudumu ili eneo hilo libakie tulivu na watu wake waweze kupata fursa ya utulivu utakjaowasaidia kushiriki katika kazi zao za kila siku.
 
Akifunga mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema ni wakati sasa nchi za Maziwa Makuu kutambua na kuazimia kwa kauli moja kuwa amani inahitajika katika nchi zote za ukanda huu. Akifafanua zaidi Mheshimiwa Rais Kenyatta alisema wananchi wa ukanda huu wanataka ajira na sio mapigano. 
 
“Hata vijana wanaotumika katika mapigano, tukumbuke kuwa baada ya mapigano watakachohitaji ni ajira. Akina mama na watoto wanataka kuona maisha yao yanaboreshwa na sio vionginevyo. Kwa namna nilivyoona tukishiriki katika mkutano huu ni dhaihiri tumeonesha nia ya dhati ya kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa na amani. Tudumishe nia hii nzuri,” alisema Rais Kenyatta.
 
Makamu wa Rais na msafara wake wanarejea nyumbani leo Alhamisi Agosti Mosi, 2013 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MAMA WA WATOTO WAWILI WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA WALIOLAZA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI NAIROBI.


Thursday, August 1, 2013

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao.

KESI YA WEMA SEPETU YAPIGWA KARENDA HADI AUG 20

Thursday, August 1, 2013


Kesi ya jinai inayomkabili muigizaji Wema Sepetu, ya tuhuma za kumpiga vibao vitano meneja wa hoteli ya Mediterano , pamoja na kuharibu mali za hoteli hiyo, imeahirishwa leo hii pia mpaka tarehe 20 mwezi wa nane.
sakata hilo lilitokea siku ya tarehe 4 mwezi wa 4, kesi yake ya kwanza ilisomwa siku ya tarehe 17, na kuahirishwa mpaka leo hii, na baada ya kufika mahakamani leo hii na Wema kukataa mashtaka hayo, kesi imeahirishwa tena mpaka tarehe 20 mwezi wa 8.
"Siku ya kwanza ya keshi hiyo wanaume walikuwa wengi, lakini leo hii imekuwa tofauti, wasichana walikuwa wengi yaani marafiki zake wakiongozwa na Kajala, walifika majira ya saa mbili na robo na waliitwa sehem maalum (chemba) kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo, na keshi hiyo ilisomwa ila ilihairishwa mpaka tarehe 20/08/2013" amesema Mwahija (mwandishi wa habari wa kujitegemea)

MAABARA YA KISASA YENYE UWEZO WA KUTAMBUA MAGONJWA MAPYA NA YALE YA HATARI SANA IKIWEMO EBOLA YAZINDULIWA BAGAMOYO.


Bagamoyo 2
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI).
Bagamoyo 1

Tuesday, 30 July 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND Yingluck Shinawatra AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

Tuesday, July 30, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  akisalimiana na baadhi ya raia wa Thailkand wanaoishi nchini alipowasili katika hoteli ya Kilimanjaro Regency Hyatt jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013
kwa ziara rasmi ya siku tatu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Ikulu nwa mgeni wake  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili  leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mandhari ya bandari ya salama Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili na ujumbe wake jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.

KAIMU NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI BW JOHN MUGONDO ATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA NA KEMONDO

( Kushoto)Naibu katibu mkuu wizara ya uchukuzi akiwa na meneja wa bandari ya bukoba  bw Ernest nyambo akimueleza jambo kuhusiana na shughuli mbalimbali za kila siku katika bandari ya bukoba
                                                              naona mambo yanakwenda
 Injinia madeni kipande mwenye miwani akiangalia shughuli mbalimbali zikiendelea bandarini bukoba
     mwenye miwani ni injinia madeni kipande kaimu mkurugenzi wa m,amlaka ya bandari(TPA)
                        ni ndizi zinazosafirishwa kwenda mwanza zikiwa bandari ya bukoba
                                                                               wakisikiliza kwa umakini
 bw john mugondo akiangalia namna mteja anavyopata huduma ya tiketi bandari ya bukoba

                                       meneja wa bandari ya kemondo bw minja akisisitiza kitu
                                                            hapa mkuu kazi inakwenda vizuri
(kushoto)ni mkuu wa bandari ya kemondo bw minja akitoa maelezo kwa kaimu katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi bw John mugondo

Sunday, 28 July 2013

RAIS KIKWETE AKIWA WILAYANI KARAGWE

Rais Kikwete akihutubia umati Ngara.
Rais Kikwete akisalimia wananchi Rulenge.

Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu.

Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa.

Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu Jumamosi Julai 27, 2013.