Thursday 13 June 2013

NI TEKNOLOGIA INAYOTUMIKA KUKAMATA SENENE,LAKINI YENYE KUITAJI GHARAMA



 Unapozungumzia senene kwa muhaya ni kitu kikubwa na cha heshima,miaka ya huko nyuma sana kipindi cha msimu wa senene nazungumzia mwezi wanne na mwezi wa kumi na moja mpaka kumi na mbili kila mwaka senene walikuwa wakipatikana kwenye mbuga zenye nyasi,hivyo watu walikwenda maeneo hayo kipindi cha msimu na kuwatafuta senene,na miaka hiyo watu walitembea mwendo mrefu sana kufuata senene maana si mbuga zote ungeweza kuwapata, kadri siku zilivyozidi kwenda binadamu wanakuwa wabunifu,na miaka ya tisini ikaingia teknologia ya kukamata senene kwa kutumia mtambo maalumu kama wanavyosema wahusika. teknologia hiyo yenye kutumia taa zenye mwanga mkali sana zinafungwa kitaalamu na mapipa ambayo senene wanapofuata mwanga uanguka kwenye mapipa hayo,staili hii inakuwa kwa kasi kubwa wakati wa msimu,lakini ni tekenologia inayohitaji pesa ili uweze kununua vifaa.wapo baadhi wanaofanya biashara hii wananunua mpaka jenereta binafsi kuepuka umeme wa tanesco,kwa kiasi kikubwa watu wamefanikiwa kujenga majumba mazuri,kusomesha watoto,kununua magari nakuendeleza biashara zao.


 ni  jenereta zinazotumika wakati wa msimu wa senene,kuepuka gharama za umeme wa tanesco



 ni mapipa ambayo senene wanapofuata mwanga na kuwa wengi hudondoka kwenye mapipa hayo


 hizo ni taa ambazo zimetolewa kioo cha nje,taa hizi uhuzwa dukani kati ya laki moja mpaka laki moja na nusu kwa taa moja


wengi wameboresha maisha yao kwa ajili ya teknologia hii ya kukamata senene,kwa bukoba eneo las nyamkazi ni maarufu kwa mitambo hii,lakini pia teknologia hii imeshasambaa katika wilaya za mkoa wa kagera na nchi jirani kama uganda, rwanda nk,leo ukizunguza senene  makabila mengi wanakula kuliko hata wahaya,na kipindi cha msibu biashara ya nyama na samaki hudorola kwani watu wengi hutumia senene kama mboga.

No comments:

Post a Comment