Sunday, 9 June 2013

MAMBO MENGI KATIKA UTAMADUNI WA MUHAYA HAYAFANYIKA KAMA ZAMANI KUTOKANA NA HALI YA MAISHA KUBADIRIKA


Enzi za mababu zetu,nyumba nyingi maeneo ya vijijini bukoba ilikuwa ni jambo la kawaida kukuta (OBWATO) mtumbwi wa kutengeneza pombe ya kienyeji orubisi kwa maana kila wiki ilikuwa ni kawaida kwenda kwa wazee tofautitofauti na kukuta wametengeneza pombe hiyo ya kienyeji, rubis inatengenezwa kwa ndizi mbivu,zinachangaywa na mtama. Miaka ya sabini wahaya chakula chao kikuu ilikuwa ni ndizi, ugari mtu alikula kwa kupenda na kwa nadra sana,na mtu alipokula ugari wengi walimshangaa na kumuona mtu mwenye dhiki hivi..,yote hiyo ilisababishwa na neema ya mashamba mazuri yenye rutuba na ndizi nyingi,zilikuwepo ndizi aina ya embile ndizo zilitumika kwa ajili ya kutengeneza pombe,aina ya ndizi hiyo ilikuwa ni marufuku kwa matumizi ya chakula, lakini mambo hubadilika leo migomba maeneo mengi hamna tena,mingi imeshambuliwa na magonjwa na wengine wametoa kabisa migomba na kuendelea na kilimo cha kutegemea msimu kama mahindi nk,hali hiyo imesababisha mambo mengi ya asili ya muhaya kupotea kutokana na hali ya maisha na kiuchumi kubadilika,vitu kama obwato ni nadra sana kukuta watu bado wanatengeneza pombe za kienyeji,maana hata hizi ndizi za pombe watu wanakula na hazipatikani tena,wenye migomba mizuri na wachache sana anbao wanauwezo wa kugharamia mashamba.

Anaonekana mtu akichota pombe kuweka kwenye dumu

Maeneo mengi bukoba miaka ya sabini walitumia kuni kupikia chakula,kizazi hiki hata vijijini wanatumia majko ya mkaa,gesi na umeme kupikia

Na nyama ya bukoba ni tofauti na maeneo mengine ,maana ng'ombe muda wote wanakula majani fresh

Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa maeneo mengi wanapanda migomba ya kisasa kwendana na hali halisi ya udongo

Aina ya ndizi hii hujulikana zaidi kwa jina la mutwishe

Wenye uwezo kifedha na mbolea ndio wanaweza kuandaa mashamba ya migomba

Wa mama wamekaa kwenye nyasi wakizungumza,
Watu hukaa kwenye nyasi na kuendelea na mazungumzo kama kawaida

Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot

No comments:

Post a Comment