Sunday 30 August 2015

KWAYA YA MT JOHNBOSCO BUKOBA YATIMIZA MIAKA 33,JUSTUCE RUGAIBULA ACHANGIA MILIONI 20,ZAHITAJIKA MILIONI 86.6 KUANZISHA STUDIO YA KUREKODI.

 Ilikuwa ni siku kubwa na ya kihistoria kwa kwaya ya Mt Johnbosco Bukoba kutimiza miaka 33 tangu kuanzishwa kwake,liliandaliwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu na kumuabudu mungu lilishirikisha kwaya mbalimbali na vikundi vya burudani ,mgeni rasmi katika Tamasha hilo alikuwa ni Bw Justuce Rugaibura alieambatana na mkewe maarufu Graice one, mama yake mzazi, ndugu jamaa na marafiki.
 Bw Justuce Rugaibula akiwa na familia yake akitangaza mchango wake wa kusaidia uanzishwaji wa studio ya kurekodi kwa ajili ya kwaya ya Mt Johnbosco Bukoba kuondokana na gharama kubwa wanazotumia wanapokwenda kurekodi nyimbo zao nje ya Mkoa au  nje ya nchi, kiasi cha shilingi milioni 86.6 kinahitajika kwa ajili ya ufunguzi wa studio hiyo, Bw Justuce Rugaibura alichangia kiasi cha shilingi milioni 20 na kuhaidi kushilikisha rafiki zake wa karibu wa ndani ya nchi na nje ya nchi ili kiasi chote cha pesa kinachohitajika kiweze kupatikana.
 Mwenyekiti wa kwaya ya Mt Johnbosco Bukoba Bw James .P. Rugaimukamu akitoa neno la kuwakaribisha wageni.
 Kwaya ya Mt Johnbosco Bukoba wakitumbuiza.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Shangwe na vifijo vilitawala pale mgeni rasmi alipotamka kuchangia kiasi cha milioni 20 na kutafuta wafadhili wengine.
 Mrs Justuce Rugaibura(kulia) katika ubora wake na tabasamu pale mzee anapofanya mambo ya msingi kwa jamii na mambo ya kumpendeza mungu.
 Hapana chezea Kwaya ya Mt Johnbosco Bukoba na hasa wakiwa jukwaani.
 Pongezi nyingi zikatolewa kwa mgeni rasmi,kitu 20 m si mchezo na hasa ukizingatia watu wanapeleka hati za nyumba benki ndio wapewe,Bw Justuce Rugaibura ni mfano wa kuigwa, kutoa ni moyo....
 Mzee kipingiri katika ubora wake.
 Wafadhili mbalimbali wakachangia.

jamcoblog.inawapongeza kwaya ya Mt Johnbosco kwa kutimiza miaka 33 kwa kuanzishwa kwake, endelea kufuatilia kwa matukio mengine ukurasa wetu wa facebook.