Tuesday 11 October 2016

HONGERA SHIRIKA LA NYUMBA,KWA KUTAMBUA TATIZO LA TETEMEKO KWA WAPANGAJI WENU BUKOBA.

 Camera yetu imepita mitaa mbalimbali katika manisipaa ya Bukoba ,ikiwa ni takribani mwezi mmoja sasa tangu litokee tetemeko la kihistoria katika mkoa wa Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya watu, maeneo ya biashara na wengine kupoteza maisha. Mpiga picha wetu akiwa katika mitaa alikutana na mhanga aliejitambulisha kwa jina moja Gozi maeneo ya soko kuu  alisema ameushukuru uongozi wa shirika la nyumba Bukoba kwa namna walivyotambua umuhimu wa wapangaji wao, baada ya kuzungumza na wafanyabiashara wapangaji wamekubaliana kukarabati kwa haraka  majengo yao yalioathilika na sasa ujenzi unaendelea vizuri.
 Moja ya jengo la NHC ambalo ukarabati wake unaendelea vizuri.

MAZISHI YA MAREHEMU GOSBERT IJUMBA ,KANYIGO NYANGOMA BUKOBA.

 Ni safari ya mwisho hapa dunia ya marehemu Gosbert Ijumba,ndugu ,jamaa na marafiki walifika katika kijiji cha Nyangoma Kanyigo kushiriki mazishi, Watu kutoka maeneo tofauti walifika,Muonekano tu wa mazishi ungekupa picha na kujifunza marehemu aliishi vipi hapa duniani,Katika mahubiri ya padre alimzungumza marehemu namna alivyojitoa kwenye mambo ya kanisa, ila yawezekana kabisa mimi na wewe tusiamini kama marehemu alijihusisha sana katika kanisa, lakini ukirudi katika maisha ya kawaida  walionekana waume kwa wake, vijana kwa wazee wote wakilia na kusikitika kifo cha Gosbert Ijumba.(katika picha mjane wa marehemu Stella Nyamwihura akiwa na wanae)