Saturday 10 September 2016

BUWASA WAPATA BODI MPYA,SAMORA LYAKULWA APATA SHAVU TENA.

Mkuu wa mkoa Kagera meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu leo tarehe 9-9-2016 ameizindua rasmi bodi mpya ya mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira manispaa ya Bukoba(BUWASA) kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Bukoba,Awali mwenyekiti mteule Bw Samora Lyakulwa akisoma taarifa kwa mgeni rasmi alisema mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za miundombinu, watu kuharibu na kujenga kwenye vyanzo vya maji,wizi wa maji, upoteaji wa maji kwa kiwango kikubwa unaosababishwa na mivujo na upasukaji wa mabomba,pia madeni makubwa wanayodai kwa wateja, taasisi mbalimbali za serikali yanayofikia zaidi ya milioni 500,Bw Samora amemuomba mgeni rasmi kuwasaidia kuhimiza wadaiwa kulipa na hasa taasisi za serikali ili fedha hizo ziweze kuboresha mamlaka, zaidi ya milioni mia mbili ni madeni ya taasisi za serikali, Mgeni rasmi wakati akizumgumza na waalikwa alizindua bodi mpya ya maji na kuwataka kufanya kazi kwa kasi zaidi ili waendane na kauli mbiu ya hapa kazi tu, na amehaidi kusaidia  kuongea na wadaiwa wote kwa upande wa serikali.Bw Samora Lyakulwa ameteuliwa tena na waziri mwenye dhamana baada ya kumaliza kipindi kilichopita cha miaka mitatu  na sasa kuteuliwa tena kwa kipindi cha miaka mitatu.(Katika picha mwenyekiti mteule Bw Samora Lyakulwa akiongea na waalikwa.)
Kushoto Mstahiki meya Manispaa ya Bukoba Chiefu Kalumuna akiwa na mkuu wa wilaya Bukoba, na katikati Mh Diwani Mwakyoma wa kata Bakoba.
Kulia Bw Samora akiwa na mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka.
Mgeni rasmi akiingia ukumbini.
Wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao.
Wajumbe waliomaliza muda wao.
Kulia Bw Karulama mjumbe aliemaliza muda wake.
Wajumbe wapya wa Bodi.
Mc wa Hafla Bi Joyce Robozi.
Waalikwa.
Kulia Mwenyekiti mteuli wa bodi akiwa na mkuu wa mkoa Kagera.
Mkurugenzi wa Buwasa akiongea jambo.
Kulia ni Mhandisi Chagaka aliestaafu akipokea cheti cha shukrani katika utumishi wake katika bodi iliyomaliza muda wake.
Mama akimpongeza baba kwa kustaafu salama.
Wajumbe wa bodi mpya wakipokea vitendea kazi kutoka kwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akitoa hotuba yake.